Ezekiel 45:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nyinyi watawala wa Israeli, mmefanya dhambi vyakutosha. Acheni ukatili na dhuluma. Tendeni mambo ya haki na sawa. Acheni kuwafukuza watu wangu nchini; mimi Bwana Mungu nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Yatosha, enyi wakuu wa Israeli! Acheni mbali ukatili wenu na uonevu wenu mkafanye lile lililo haki na sawa. Acheni kuwatoza watu wangu isivyo haki, asema Bwana Mungu Mwenyezi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana MUNGU asema hivi; Na iwatoshe ninyi, enyi wakuu wa Israeli; ondoeni dhuluma na unyang'anyi; fanyeni hukumu na haki; ondoeni kutoza kwa nguvu kwenu katika watu wangu, asema Bwana MUNGU.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nyinyi watawala wa Israeli, mmefanya dhambi vyakutosha. Acheni ukatili na dhuluma. Tendeni mambo ya haki na sawa. Acheni kuwafukuza watu wangu nchini; mimi Bwana Mungu nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Yatosha, enyi wakuu wa Israeli! Acheni mbali ukatili wenu na uonevu wenu mkafanye lile lililo haki na sawa. Acheni kuwatoza watu wangu isivyo haki, asema BWANA Mwenyezi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Yatosha, enyi wakuu wa Israeli! Acheni mbali ukatili wenu na uonevu wenu mkafanye lile lililo haki na sawa. Acheni kuwatoza watu wangu isivyo haki, asema bwana Mwenyezi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bwana MUNGU asema hivi; Na iwatoshe ninyi, enyi wakuu wa Israeli; ondoeni dhuluma na unyang'anyi; fanyeni hukumu na haki; acheni kutoza kwenu kwa nguvu katika watu wangu, asema Bwana MUNGU.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nyinyi watawala wa Israeli, mmefanya dhambi vyakutosha. Acheni ukatili na dhuluma. Tendeni mambo ya haki na sawa. Acheni kuwafukuza watu wangu nchini; mimi Bwana Mungu nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mabaya yenu, mliyoyafanya ninyi wakuu wa Isiraeli, ni mengi; kwa hiyo acheni ukorofi na unyang'anyi, mpige mashauri yaliyo sawa yaongokayo, msiwafukuze kwao tena walio ukoo wangu! ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bwana MUNGU asema hivi; Na iwatoshe ninyi, enyi wakuu wa Israeli; ondoeni dhuluma na unyang’anyi; fanyeni hukumu na haki; ondoeni kutoza kwa nguvu kwenu katika watu wangu, asema Bwana MUNGU.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana wetu Yawe anasema hivi: Ninyi wakubwa wa Waisraeli, mumefanya zambi vyakutosha. Muache kutesa watu kwa ukali. Muimarishe sheria yangu na haki. Muache kuwafukuza watu wangu katika inchi. –Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe.–