Ezekiel 46:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtawala anapotaka kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka kwa hiari, iwe sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani, watamfungulia lango la ukumbi wa ndani unaoelekea mashariki. Atatoa sadaka kama anavyofanya siku ya sabato, na anapotoka, lango lifungwe nyuma yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkuu anayetawala anapotoa sadaka ya hiari kwa Mwenyezi Mungu, iwe ni sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani, atafunguliwa lango linaloelekea mashariki. Atatoa sadaka yake ya kuteketezwa au sadaka yake ya amani kama afanyavyo katika siku ya Sabato. Kisha atatoka nje. Baada yake kutoka nje, lango litafungwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye mkuu atakapotengeneza sadaka atoayo kwa hiari yake mwenyewe, sadaka ya kuteketezwa, au sadaka za amani, ziwe sadaka amtoleazo Bwana kwa hiari yake mwenyewe, mtu mmoja atamfungulia lango lile lielekealo upande wa mashariki, naye ataitengeneza sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka zake za amani, kama afanyavyo siku ya sabato; kisha atatoka; na baada ya kutoka kwake mtu mmoja atalifunga lango.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtawala anapotaka kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka kwa hiari, iwe sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani, watamfungulia lango la ukumbi wa ndani unaoelekea mashariki. Atatoa sadaka kama anavyofanya siku ya sabato, na anapotoka, lango lifungwe nyuma yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mkuu anayetawala anapotoa sadaka ya hiari kwa BWANA, ikiwa ni sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani, lango linaloelekea mashariki litafunguliwa kwa ajili yake. Atatoa sadaka yake ya kuteketezwa au sadaka yake ya amani kama afanyavyo katika siku ya Sabato. Kisha atatoka nje, naye akiisha kutoka nje, lango litafungwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mkuu anayetawala anapotoa sadaka ya hiari kwa bwana, ikiwa ni sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani, lango linaloelekea mashariki litafunguliwa kwa ajili yake. Atatoa sadaka yake ya kuteketezwa au sadaka yake ya amani kama afanyavyo katika siku ya Sabato. Kisha atatoka nje, naye akiisha kutoka nje, lango litafungwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye mkuu atakapotengeneza sadaka atoayo kwa hiari yake mwenyewe, sadaka ya kuteketezwa, au sadaka za amani, ziwe sadaka amtoleazo BWANA kwa hiari yake mwenyewe, mtu mmoja atamfungulia lango lile lielekealo upande wa mashariki, naye ataitoa sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka zake za amani, kama afanyavyo siku ya sabato; kisha atatoka; na baada ya kutoka kwake mtu mmoja atalifunga lango.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtawala anapotaka kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka kwa hiari, iwe sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani, watamfungulia lango la ukumbi wa ndani unaoelekea mashariki. Atatoa sadaka kama anavyofanya siku ya sabato, na anapotoka, lango lifungwe nyuma yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama mkuu anataka kumtolea Bwana kwa kupenda mwenyewe ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima au za kushukuru, basi, wamfungulie lile lango lielekealo maawioni kwa jua, azitoe ng'ombe zake za tambiko za kuteketezwa nzima nazo za kushukuru, kama anavyofanya siku za mapumziko, kisha atoke! Akiisha kutoka, na walifunge hilo lango.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye mkuu atakapotengeneza sadaka atoayo kwa hiari yake mwenyewe, sadaka ya kuteketezwa, au sadaka za amani, ziwe sadaka amtoleazo BWANA kwa hiari yake mwenyewe, mtu mmoja atamfungulia lango lile lielekealo upande wa mashariki, naye ataitengeneza sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka zake za amani, kama afanyavyo siku ya sabato; kisha atatoka; na baada ya kutoka kwake mtu mmoja atalifunga lango.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme anapotaka kumutolea Yawe sadaka kwa mapenzi yake, ikiwa ni sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani, watamufungulia mulango wa kiwanja cha ndani unaoelekea upande wa mashariki. Atatoa sadaka kama anavyofanya siku ya Sabato, na anapotoka, mulango ufungwe nyuma yake.