Ezekiel 46:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kila siku asubuhi mtamtolea Mwenyezi-Mungu mwanakondoo wa mwaka mmoja asiye na dosari, ambaye atateketezwa mzima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Kila siku utamtoa mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiyekuwa na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa Mwenyezi Mungu, utaitoa kila siku asubuhi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe utatengeneza mwana-kondoo wa mwaka wa kwanza, mkamilifu, kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana kila siku; kila siku asubuhi utamtengeneza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kila siku asubuhi mtamtolea Mwenyezi-Mungu mwanakondoo wa mwaka mmoja asiye na dosari, ambaye atateketezwa mzima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Kila siku utamtoa mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiyekuwa na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA, utaitoa kila siku asubuhi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Kila siku utamtoa mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiyekuwa na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa bwana, utaitoa kila siku asubuhi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe utamtoa mwana-kondoo wa mwaka mmoja, mkamilifu, kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA kila siku; kila siku asubuhi utamtoa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kila siku asubuhi mtamtolea Mwenyezi-Mungu mwanakondoo wa mwaka mmoja asiye na dosari, ambaye atateketezwa mzima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe umtolee Bwana kila siku mwana kondoo wa mwaka mmoja asiye na kilema kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima, ufanye hivyo kila kutakapokucha!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe utatengeneza mwana-kondoo wa mwaka wa kwanza, mkamilifu, kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA kila siku; kila siku asubuhi utamtengeneza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila siku asubui mutamutolea Yawe mwana-kondoo wa mwaka mumoja asiyekuwa na kilema, ambaye atateketezwa kwa moto.