Ezekiel 46:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pia kila siku, sadaka ya kilo mbili za unga itatolewa asubuhi pamoja na lita moja ya mafuta ya zeituni yakichanganywa na unga. Ni lazima kufuata sheria za sadaka hii kwa Mwenyezi-Mungu milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia kila siku asubuhi pamoja na hiyo sadaka utatoa sadaka ya nafaka, ikiwa na sehemu ya sita ya efa pamoja na theluthi moja ya hini ya mafuta ya kuchanganya na ule unga. Utoaji wa sadaka hii ya nafaka kwa Mwenyezi Mungu ni agizo la kudumu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe utatengeneza sadaka ya unga pamoja nayo kila siku asubuhi, sehemu ya sita ya efa moja, na sehemu ya tatu ya hini moja ya mafuta; kuchanganya na unga ule mzuri; sadaka ya unga kwa Bwana daima, kwa amri ya milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pia kila siku, sadaka ya kilo mbili za unga itatolewa asubuhi pamoja na lita moja ya mafuta ya zeituni yakichanganywa na unga. Ni lazima kufuata sheria za sadaka hii kwa Mwenyezi-Mungu milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia kila siku asubuhi pamoja na hiyo sadaka utatoa sadaka ya nafaka, ikiwa na sehemu ya sita ya efa pamoja na theluthi moja ya hini ya mafuta ya kuchanganya na ule unga. Utoaji wa sadaka hii ya nafaka kwa BWANA ni amri ya daima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia kila siku asubuhi pamoja na hiyo sadaka utatoa sadaka ya nafaka, ikiwa na sehemu ya sita ya efa pamoja na theluthi moja ya hini ya mafuta ya kuchanganya na ule unga. Utoaji wa sadaka hii ya nafaka kwa bwana ni amri ya daima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe utaitoa sadaka ya unga pamoja nayo kila siku asubuhi, sehemu ya sita ya efa moja, na sehemu ya tatu ya hini moja ya mafuta; kuchanganya na unga ule mzuri; sadaka ya unga kwa BWANA daima, kwa amri ya milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pia kila siku, sadaka ya kilo mbili za unga itatolewa asubuhi pamoja na lita moja ya mafuta ya zeituni yakichanganywa na unga. Ni lazima kufuata sheria za sadaka hii kwa Mwenyezi-Mungu milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata kilaji cha tambiko sharti ukitoe kila kutakapokucha, kiwe pishi moja ya unga na vibaba viwili vya mafuta ya kumiminiwa katika huo unga uliopepetwa vizuri. Hiki kilaji cha tambiko cha Bwana kimeagizwa cha siku zote za kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe utatengeneza sadaka ya unga pamoja nayo kila siku asubuhi, sehemu ya sita ya efa moja, na sehemu ya tatu ya hini moja ya mafuta; kuchanganya na unga ule mzuri; sadaka ya unga kwa BWANA daima, kwa amri ya milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile kila siku, sadaka ya kilo mbili za unga itatolewa asubui pamoja na litre moja ya mafuta ya muzeituni yakichanganywa na unga. Inafaa kufuata maagizo za sadaka hii kwa Yawe milele.