Ezekiel 46:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtawala kamwe asipore mali ya watu. Ardhi yoyote anayowapa watoto wake wa kiume ni lazima itokane na eneo lake mwenyewe. Hivyo hatawadhulumu watu wangu kwa kuwanyanganya ardhi yao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkuu anayetawala hafai kuchukua urithi wowote wa watu na kuwaondoa kwenye mali yao. Mkuu huyo atawapa wanawe urithi wao katika mali yake mwenyewe, ili pasiwe na mtu wangu yeyote atakayetengwa na urithi wake.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mkuu hatawaondolea watu urithi wao, hata kuwatoa kwa nguvu katika milki yao; atawapa wanawe urithi katika mali yake mwenyewe, watu wangu wasije wakatawanyika, kila mtu mbali na milki yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtawala kamwe asipore mali ya watu. Ardhi yoyote anayowapa watoto wake wa kiume ni lazima itokane na eneo lake mwenyewe. Hivyo hatawadhulumu watu wangu kwa kuwanyang'anya ardhi yao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mkuu anayetawala hana ruhusa kuchukua urithi wo wote wa watu na kuwaondoa kwenye mali zao. Mkuu atawalaye atawapa wanawe urithi wao, kutoka kwenye mali zake mwenyewe, ili kwamba pasiwe na mtu wangu ye yote atakayetengwa na urithi wake.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mkuu anayetawala hana ruhusa kuchukua urithi wowote wa watu na kuwaondoa kwenye mali zao. Mkuu atawalaye atawapa wanawe urithi wao, kutoka kwenye mali zake mwenyewe, ili kwamba pasiwe na mtu wangu yeyote atakayetengwa na urithi wake.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mkuu hatawaondolea watu urithi wao, hata kuwatoa kwa nguvu katika milki yao; atawapa wanawe urithi katika mali yake mwenyewe, watu wangu wasije wakatawanyika, kila mtu mbali na milki yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtawala kamwe asipore mali ya watu. Ardhi yoyote anayowapa watoto wake wa kiume ni lazima itokane na eneo lake mwenyewe. Hivyo hatawadhulumu watu wangu kwa kuwanyanganya ardhi yao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena mkuu asichukue fungu lililo la watu akiwakorofisha na kuwafukuza kwao. Lililo lake ni fungu lile tu, alilopewa kulishika, liwe lake, nalo ndilo, atakaloachia wanawe, kusudi walio ukoo wangu wasitawanyike, mtu akiweza kuondolewa katika fungu, alilolishika, liwe lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mkuu hatawaondolea watu urithi wao, hata kuwatoa kwa nguvu katika milki yao; atawapa wanawe urithi katika mali yake mwenyewe, watu wangu wasije wakatawanyika, kila mtu mbali na milki yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme hapaswi kunyanganya hata kidogo mali ya watu. Sehemu ya inchi yoyote anayowapa watoto wake wa kiume inapaswa kutokana na eneo lake mwenyewe. Hivyo hatawatesa watu wangu kwa kuwanyanganya urizi wao.