Ezekiel 46:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Toka nje, mtawala ataingia ukumbi wa ndani kwa kupitia lango la ukumbi huo. Naye atasimama karibu na nguzo ya lango, wakati makuhani wanateketeza sadaka zake za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha mtawala huyo atasujudia kwenye lango na baadaye atatoka nje. Lango litabaki wazi hadi jioni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkuu anayetawala ataingia kupitia baraza ya njia ya lango la ukumbi na kusimama karibu na nguzo ya lango. Makuhani watatoa sadaka za mkuu anayetawala za kuteketezwa na sadaka za amani. Mkuu anayetawala atasujudu kwenye kizingiti cha njia ya lango, kisha atatoka nje, lakini lango halitafungwa hadi jioni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye mkuu ataingia kwa njia ya ukumbi wa lango lile, upande wa nje, naye atasimama karibu na mwimo wa lango, nao makuhani wataitengeneza sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka zake za amani, naye ataabudu penye kizingiti cha lango; kisha atatoka; lakini lango lile halitafungwa hata wakati wa jioni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Toka nje, mtawala ataingia ukumbi wa ndani kwa kupitia lango la ukumbi huo. Naye atasimama karibu na nguzo ya lango, wakati makuhani wanateketeza sadaka zake za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha mtawala huyo atasujudia kwenye lango na baadaye atatoka nje. Lango litabaki wazi hadi jioni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mkuu anayetawala ataingia kupitia baraza ya njia ya lango la ukumbi na kusimama karibu na nguzo ya lango. Makuhani watatoa sadaka za mkuu anayetawala za kuteketezwa na sadaka za amani. Mkuu anayetawala atasujudu kwenye kizingiti cha njia ya lango, kisha atatoka nje, lakini lango halitafungwa mpaka jioni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mkuu anayetawala ataingia kupitia baraza ya njia ya lango la ukumbi na kusimama karibu na nguzo ya lango. Makuhani watatoa sadaka za mkuu anayetawala za kuteketezwa na sadaka za amani. Mkuu anayetawala atasujudu kwenye kizingiti cha njia ya lango, kisha atatoka nje, lakini lango halitafungwa mpaka jioni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye mkuu ataingia kwa njia ya ukumbi wa lango lile, upande wa nje, naye atasimama karibu na mwimo wa lango, nao makuhani wataitengeneza sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka zake za amani, naye ataabudu penye kizingiti cha lango; kisha atatoka; lakini lango lile halitafungwa hadi wakati wa jioni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Toka nje, mtawala ataingia ukumbi wa ndani kwa kupitia lango la ukumbi huo. Naye atasimama karibu na nguzo ya lango, wakati makuhani wanateketeza sadaka zake za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha mtawala huyo atasujudia kwenye lango na baadaye atatoka nje. Lango litabaki wazi hadi jioni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mkuu akiingia penye ukumbi wa hilo lango toka nje, asimame hapo penye mhimili wa hilo lango, watambikaji waitengeneze ng'ombe yake ya tambiko ya kuteketezwa nzima nazo ng'ombe za tambiko za kushukuru, naye amwangukie Mungu penye kizingiti cha hilo lango, kisha atoke; kisha lango hilo lisifungwe mpaka jioni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye mkuu ataingia kwa njia ya ukumbi wa lango lile, upande wa nje, naye atasimama karibu na mwimo wa lango, nao makuhani wataitengeneza sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka zake za amani, naye ataabudu penye kizingiti cha lango; kisha atatoka; lakini lango lile halitafungwa hata wakati wa jioni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tokea inje, mufalme ataingia katika baraza ya ndani kwa kupitia kwenye mulango wa baraza hiyo. Naye atasimama karibu na nguzo ya mulango, wakati makuhani wanateketeza sadaka zake za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani. Kisha mufalme huyo atainama chini kwenye mulango kwa kuabudu na kisha atatoka inje. Mulango utabaki wazi mpaka magaribi.