Ezekiel 46:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku ya sabato, mtawala atamletea Mwenyezi-Mungu wanakondoo sita na kondoo dume mmoja, wote wasio na dosari, kama sadaka ya kuteketezwa nzima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sadaka za kuteketezwa aletazo mkuu anayetawala kwa Mwenyezi Mungu siku ya Sabato zitakuwa ni wana-kondoo sita na kondoo dume mmoja, wote wasiwe na dosari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nayo sadaka ya kuteketezwa, ambayo mkuu atamtolea Bwana siku ya sabato, itakuwa wana-kondoo sita wakamilifu, na kondoo mume mkamilifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku ya sabato, mtawala atamletea Mwenyezi-Mungu wanakondoo sita na kondoo dume mmoja, wote wasio na dosari, kama sadaka ya kuteketezwa nzima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sadaka ya kuteketezwa aletazo mkuu anayetawala kwa BWANA siku ya Sabato itakuwa ni wana-kondoo sita na kondoo dume mmoja, wote wasiwe na dosari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sadaka ya kuteketezwa aletazo mkuu anayetawala kwa bwana siku ya Sabato itakuwa ni wana-kondoo sita na kondoo dume mmoja, wote wasiwe na dosari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nayo sadaka ya kuteketezwa, ambayo mkuu atamtolea BWANA siku ya sabato, itakuwa wana-kondoo sita wakamilifu, na kondoo dume mkamilifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku ya sabato, mtawala atamletea Mwenyezi-Mungu wanakondoo sita na kondoo dume mmoja, wote wasio na dosari, kama sadaka ya kuteketezwa nzima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nazo ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, mkuu atakazomtolea Bwana siku za mapumziko, ziwe wana kondoo sita wasio na kilema na dume mmoja asiye na kilema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nayo sadaka ya kuteketezwa, ambayo mkuu atamtolea BWANA siku ya sabato, itakuwa wana-kondoo sita wakamilifu, na kondoo mume mkamilifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya Sabato, mufalme ataleta kwa Yawe wana-kondoo sita na kondoo dume mumoja wote wasiokuwa na kilema kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto.