Ezekiel 46:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pamoja na kila fahali na kila kondoo dume anayetolewa sadaka, ni lazima pawepo lita kumi na saba na nusu za unga, na pamoja na kila mwanakondoo, ni lazima pawepo chochote ambacho mtawala anatoa. Tena kwa kila sadaka ya nafaka, ni lazima kutoa lita tatu za nafaka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atatoa sadaka ya nafaka ya: efa moja kwa huyo fahali, na efa moja kwa huyo kondoo dume; na kwa wana-kondoo atatoa nafaka nyingi kama atakavyo kutoa; atatoa hini ya mafuta kwa kila efa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atatengeneza sadaka ya unga, efa moja kwa ng'ombe mume, na efa moja kwa kondoo mume, na kwa wale wana-kondoo, kwa kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta kwa efa moja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pamoja na kila fahali na kila kondoo dume anayetolewa sadaka, ni lazima pawepo lita kumi na saba na nusu za unga, na pamoja na kila mwanakondoo, ni lazima pawepo chochote ambacho mtawala anatoa. Tena kwa kila sadaka ya nafaka, ni lazima kutoa lita tatu za nafaka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atatoa kuwa sadaka ya nafaka efa moja pamoja na fahali mmoja, efa moja na kondoo dume mmoja na pamoja na wana-kondoo kama atakavyo kutoa, pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atatoa kuwa sadaka ya nafaka efa moja pamoja na fahali mmoja, efa moja na kondoo dume mmoja na pamoja na wana-kondoo kama atakavyo kutoa, pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye atatengeneza sadaka ya unga, efa moja kwa ng'ombe dume, na efa moja kwa kondoo dume, na kwa wale wana-kondoo, kwa kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta kwa efa moja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pamoja na kila fahali na kila kondoo dume anayetolewa sadaka, ni lazima pawepo lita kumi na saba na nusu za unga, na pamoja na kila mwanakondoo, ni lazima pawepo chochote ambacho mtawala anatoa. Tena kwa kila sadaka ya nafaka, ni lazima kutoa lita tatu za nafaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Frasila moja ya unga kwa yule ndama, tena frasila moja ya yule dume la kondoo iwe kilaji cha tambiko, nacho cha wana kondoo kiwe, kama mkono wake utakavyoleta, tena kwa kila frasila ya unga pishi moja na nusu ya mafuta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atatengeneza sadaka ya unga, efa moja kwa ng’ombe mume, na efa moja kwa kondoo mume, na kwa wale wana-kondoo, kwa kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta kwa efa moja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pamoja na kila ngombe dume na kila kondoo dume anayetolewa sadaka, kunapaswa kuwa litre kumi na saba na nusu za unga, na pamoja na kila mwana-kondoo, kunapaswa kuwa chochote ambacho mufalme anatoa. Tena kwa kila sadaka ya unga, kunapaswa kutolewa litre tatu za unga.