Ezekiel 46:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wanapokuja kumwabudu Mwenyezi-Mungu wakati wa sikukuu yoyote, wale walioingia kwa njia ya lango la kaskazini, watatoka kwa njia ya lango la kusini; na wale walioingia kwa lango la kusini, watatoka kwa njia ya lango la kaskazini. Mtu asirudi kwa njia ya lango aliloingilia, bali atatoka kwa njia ya lango lililo mbele yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Watu wa nchi wanapokuja mbele za Mwenyezi Mungu katika sikukuu zilizoamriwa, yeyote aingiaye kwa lango la kaskazini kuabudu atatoka nje kwa lango la kusini; na yeyote aingiaye kwa lango la kusini atatoka nje kwa lango la kaskazini. Hakuna mtu yeyote atakayerudi kupitia lango lile aliloingilia, lakini kila mmoja atatoka nje kwa lango linalokabili lile aliloingilia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini watu wa nchi watakapokuja mbele za Bwana katika sikukuu zilizoamriwa, yeye aingiaye kwa njia ya lango la upande wa kaskazini ili kuabudu, atatoka kwa njia ya lango la upande wa kusini; na yeye aingiaye kwa njia ya lango la upande wa kusini, atatoka kwa njia ya lango la upande wa kaskazini; hatarudi kwa njia ya lango aliloingia kwalo, lakini atatoka kwa kwenda mbele moja kwa moja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wanapokuja kumwabudu Mwenyezi-Mungu wakati wa sikukuu yoyote, wale walioingia kwa njia ya lango la kaskazini, watatoka kwa njia ya lango la kusini; na wale walioingia kwa lango la kusini, watatoka kwa njia ya lango la kaskazini. Mtu asirudi kwa njia ya lango aliloingilia, bali atatoka kwa njia ya lango lililo mbele yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Wakati watu wa nchi wanapokuja mbele za BWANA katika sikukuu zilizoamriwa, ye yote aingiaye kwa lango la kaskazini kuabudu atatoka nje kwa lango la kusini na ye yote aingiaye kwa lango la kusini atatoka nje kwa lango la kaskazini. Hakuna mtu ye yote atakayerudi kwa kupitia lango lile aliloingilia, lakini kila mmoja atatoka nje kwa lango linalokabili lile aliloingilia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Wakati watu wa nchi wanapokuja mbele za bwana katika sikukuu zilizoamriwa, yeyote aingiaye kwa lango la kaskazini kuabudu atatoka nje kwa lango la kusini na yeyote aingiaye kwa lango la kusini atatoka nje kwa lango la kaskazini. Hakuna mtu yeyote atakayerudi kwa kupitia lango lile aliloingilia, lakini kila mmoja atatoka nje kwa lango linalokabili lile aliloingilia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini watu wa nchi watakapokuja mbele za BWANA katika sikukuu zilizoamriwa, yeye aingiaye kwa njia ya lango la upande wa kaskazini ili kuabudu, atatoka kwa njia ya lango la upande wa kusini; na yeye aingiaye kwa njia ya lango la upande wa kusini, atatoka kwa njia ya lango la upande wa kaskazini; hatarudi kwa njia ya lango aliloingia kwalo, lakini atatoka kwa kwenda mbele moja kwa moja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wanapokuja kumwabudu Mwenyezi-Mungu wakati wa sikukuu yoyote, wale walioingia kwa njia ya lango la kaskazini, watatoka kwa njia ya lango la kusini; na wale walioingia kwa lango la kusini, watatoka kwa njia ya lango la kaskazini. Mtu asirudi kwa njia ya lango aliloingilia, bali atatoka kwa njia ya lango lililo mbele yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini watu wa nchi hii wakimtokea Bwana kumwangukia penye mikutano ya sikukuu, wao walioingia katika lango la kaskazini sharti watoke penye lango la kusini, nao walioingia katika lango la kusini sharti watoke penye lango la kaskazini, mtu asirudi kwa njia ya lango lile, aliloliingia, ila atoke kwa lile la ng'ambo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini watu wa nchi watakapokuja mbele za BWANA katika sikukuu zilizoamriwa, yeye aingiaye kwa njia ya lango la upande wa kaskazini ili kuabudu, atatoka kwa njia ya lango la upande wa kusini; na yeye aingiaye kwa njia ya lango la upande wa kusini, atatoka kwa njia ya lango la upande wa kaskazini; hatarudi kwa njia ya lango aliloingia kwalo, lakini atatoka kwa kwenda mbele moja kwa moja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wanapokuja kumwabudu Yawe wakati wa sikukuu yoyote, wale walioingia kwa njia ya mulango wa kaskazini, watatoka kwa njia ya mulango wa kusini; na wale walioingia kwa mulango wa kusini, watatoka kwa njia ya mulango wa kaskazini. Mutu asirudi kwa njia ya mulango alioingilia, lakini atatoka kwa njia ya mulango unaokuwa mbele yake.