Ezekiel 47:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wavuvi watasimama ufuoni mwa bahari, na eneo kutoka Engedi mpaka En-eglaimu litakuwa la kuanikia nyavu zao. Kutakuwa na aina nyingi za samaki kama zilivyo katika Bahari ya Mediteranea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wavuvi watasimama kando ya bahari; kuanzia En-Gedi hadi En-Eglaimu kutakuwa mahali pa kutandaza nyavu za kuvulia samaki. Samaki watakuwa wa aina nyingi, kama samaki wa Bahari Kuu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena itakuwa, wavuvi watasimama karibu nao; toka Engedi mpaka En-eglaimu, patakuwa ni mahali pa kutandazia nyavu; samaki wao watakuwa namna zao mbalimbali, kama samaki wa bahari kubwa, wengi sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wavuvi watasimama ufuoni mwa bahari, na eneo kutoka Engedi mpaka En-eglaimu litakuwa la kuanikia nyavu zao. Kutakuwa na aina nyingi za samaki kama zilivyo katika Bahari ya Mediteranea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wavuvi watasimama kando ya bahari, kuanzia En-Gedi hadi En-Eglaimu huko patakuwa mahali pa kutandaza nyavu za kuvulia samaki. Samaki watakuwa wa aina nyingi, kama samaki wa Bahari Kuu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wavuvi watasimama kando ya bahari, kuanzia En-Gedi hadi En-Eglaimu huko patakuwa mahali pa kutandaza nyavu za kuvulia samaki. Samaki watakuwa wa aina nyingi, kama samaki wa Bahari Kuu
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena itakuwa, wavuvi watasimama karibu nao; toka Engedi mpaka En-eglaimu, patakuwa ni mahali pa kutandazia nyavu; samaki wao watakuwa namna zao mbalimbali, kama samaki wa bahari kubwa, wengi sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wavuvi watasimama ufuoni mwa bahari, na eneo kutoka Engedi mpaka En-eglaimu litakuwa la kuanikia nyavu zao. Kutakuwa na aina nyingi za samaki kama zilivyo katika Bahari ya Mediteranea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wavuvi watakaposimama pwani pake toka En-Gedi (Chemchemi ya Wana mbuzi) mpaka En-Egilemu (Chemchemi ya Ndama), maana patakuwa mahali pa kuanikia nyavu; samaki wa hapo watakuwa wa namna zao, tena wengi sana kama samaki wa Bahari Kubwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena itakuwa, wavuvi watasimama karibu nao; toka Engedi mpaka En-eglaimu, patakuwa ni mahali pa kutandazia nyavu; samaki wao watakuwa namna zao mbalimbali, kama samaki wa bahari kubwa, wengi sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wavuvi watasimama kandokando ya bahari, na nafasi toka Engedi mpaka Eni-Eglaimu itakuwa ya kuanikia nyavu. Kutakuwa aina nyingi za samaki kama zinavyokuwa katika bahari ya Mediteranea.