Ezekiel 47:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Upande wa magharibi, mpaka ni Bahari ya Mediteranea na utapanda kaskazini hadi mahali pa kuingilia Hamathi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Upande wa magharibi, Bahari Kuu itakuwa ndio mpaka hadi kwenye sehemu mkabala na Lebo-Hamathi. Huu utakuwa mpaka wa magharibi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na upande wa magharibi, utakuwa ni bahari kubwa, kutoka mpaka wa kusini mpaka mahali penye kuelekea maingilio ya Hamathi. Huu ndio upande wa magharibi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Upande wa magharibi, mpaka ni Bahari ya Mediteranea na utapanda kaskazini hadi mahali pa kuingilia Hamathi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Upande wa magharibi, Bahari Kuu itakuwa ndio mpaka hadi kwenye sehemu mkabala na Lebo-Hamathi. Huu utakuwa ndio mpaka wa magharibi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Upande wa magharibi, Bahari Kuu itakuwa ndio mpaka hadi kwenye sehemu mkabala na Lebo-Hamathi. Huu utakuwa ndio mpaka wa magharibi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na upande wa magharibi, utakuwa ni bahari kubwa, kutoka mpaka wa kusini mpaka mahali penye kuelekea maingilio ya Hamathi. Huu ndio upande wa magharibi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Upande wa magharibi, mpaka ni Bahari ya Mediteranea na utapanda kaskazini hadi mahali pa kuingilia Hamathi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao upande wa baharini mpaka ni Bahari Kubwa toka hapo kufika ng'ambo ya Hamati; huu ndio mpaka wa upande wa baharini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na upande wa magharibi, utakuwa ni bahari kubwa, kutoka mpaka wa kusini mpaka mahali penye kuelekea maingilio ya Hamathi. Huu ndio upande wa magharibi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Upande wa magaribi, mupaka ni bahari ya Mediteranea na utapanda upande wa kaskazini mpaka pahali pa kuingilia Hamati.