Ezekiel 47:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akaniambia, “Maji haya yanatiririka kupitia nchini hadi Araba; na yakifika huko yatayafanya maji ya Bahari ya Chumvi kuwa maji mazuri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaniambia, “Haya maji yanatiririka kuelekea nchi ya mashariki na kushuka hadi Araba, ambapo huingia Baharini. Yanapomwagikia kwenye hiyo Bahari, maji hayo huponywa na kuwa safi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo akaniambia, Maji haya yanatoka kwenda pande za nchi ya mashariki, nayo yanashuka mpaka Araba, na kuingia katika bahari
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akaniambia, “Maji haya yanatiririka kupitia nchini hadi Araba; na yakifika huko yatayafanya maji ya Bahari ya Chumvi kuwa maji mazuri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaniambia, “Haya maji yanatiririka kuelekea nchi ya mashariki na kushuka mpaka Araba, ambapo huingia Baharini. Yanapomwagikia kwenye hiyo Bahari, maji yaliyoko humo huponywa na kuwa safi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaniambia, “Haya maji yanatiririka kuelekea nchi ya mashariki na kushuka mpaka Araba, ambapo huingia Baharini. Yanapomwagikia kwenye hiyo Bahari, maji yaliyoko humo huponywa na kuwa safi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo akaniambia, Maji haya yanatoka kwenda pande za nchi ya mashariki, nayo yanashuka mpaka Araba, na kuingia katika bahari; maji yatokezwayo yataingia baharini, na maji yake yatakuwa safi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akaniambia, “Maji haya yanatiririka kupitia nchini hadi Araba; na yakifika huko yatayafanya maji ya Bahari ya Chumvi kuwa maji mazuri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaniambia: Maji hayo yanatoka hapa kwenda katika nchi zilizoko upande wa maawioni kwa jua, yanashuka kwenda nyikani, yafike baharini. Tena hapo yatakapoingia baharini, yale maji ya huko yataonekana, ya kuwa yamegeuka kuwa mazuri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo akaniambia, Maji haya yanatoka kwenda pande za nchi ya mashariki, nayo yanashuka mpaka Araba, na kuingia katika bahari; maji yatokezwayo yataingia baharini, na maji yake yataponyeka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akaniambia: Maji haya yanatiririka kupitia katika inchi mpaka katika bonde la Yordani, na yakifika huko yatayafanya maji ya bahari ya Chumvi kuwa maji mazuri.