Ezekiel 47:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila mahali mto huu utakapopita, kutaishi aina zote za wanyama na samaki. Mto huu utayafanya maji ya Bahari ya Chumvi kuwa maji baridi. Kokote utakakopita utaleta uhai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Popote mto huu unatakapofika, kila kiumbe hai kinachoingia ndani ya hayo maji kitaishi. Nako kutakuwa na samaki wengi mno, mara maji haya yatakapofika huko. Maji hayo yatakuwa hai, na kila kitu kitaishi popote mto utakapofika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena itakuwa, kila kiumbe hai kisongamanacho, kila mahali itakapofika mito hiyo, kitaishi; kutakuwapo wingi mkubwa wa samaki, kwa sababu maji haya yamefika huko maana maji yale yataponyeka, na kila kitu kitaishi po pote utakapofikilia mto huo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila mahali mto huu utakapopita, kutaishi aina zote za wanyama na samaki. Mto huu utayafanya maji ya Bahari ya Chumvi kuwa maji baridi. Kokote utakakopita utaleta uhai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Po pote mto huu uendapo kila kiumbe hai kinachoyaparamia hayo maji kitaishi, nako kutakuwa na samaki wengi mno, mara maji haya yafikapo huko. Maji hayo yatakuwa hai na kila kitu kitakachoishi kule mto uendako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Popote mto huu uendapo kila kiumbe hai kinachoyaparamia hayo maji kitaishi, nako kutakuwa na samaki wengi mno, mara maji haya yafikapo huko. Maji hayo yatakuwa hai na kila kitu kitakachoishi kule mto uendako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena itakuwa, kila kiumbe hai kisongamanacho, kila mahali itakapofika mito hiyo, kitaishi; kutakuwapo wingi mkubwa wa samaki, kwa sababu maji haya yamefika huko maana maji yale yatakuwa safi, na kila kitu kitaishi popote utakapofika mto huo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila mahali mto huu utakapopita, kutaishi aina zote za wanyama na samaki. Mto huu utayafanya maji ya Bahari ya Chumvi kuwa maji baridi. Kokote utakakopita utaleta uhai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, itakapokuwa, vinyama vyote vitambaavyo hapo po pote, maji ya mto huo yatakapofika, vitapata uzima, nao samaki watakuwa hapo wengi sana, kwani maji haya yatafika hapo; ndipo, watakapopona na kupata kuwapo po pote, mto huu utakapofika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena itakuwa, kila kiumbe hai kisongamanacho, kila mahali itakapofika mito hiyo, kitaishi; kutakuwapo wingi mkubwa wa samaki, kwa sababu maji haya yamefika huko maana maji yale yataponyeka, na kila kitu kitaishi po pote utakapofikilia mto huo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila pahali muto huu utakapopita, kutaishi aina zote za nyama na samaki. Muto huu utayafanya maji ya bahari ya Chumvi kuwa maji baridi. Kokote utakakopita utaleta uzima.