Ezekiel 48:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: Kuanzia mpaka wa kaskazini kwenye barabara ya Hethloni hadi kuingia Hamathi hadi mji wa Hazar-enoni (ulioko mpakani mwa Damasko na Hamathi upande wa kaskazini na kuendelea kutoka mashariki hadi magharibi), eneo hilo litakuwa la kabila la Dani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: “Kwenye mpaka wa kaskazini, Dani atakuwa na sehemu moja; mpaka huo utafuata barabara ya Hethloni hadi Lebo-Hamathi; Hasar-Enani hata mpaka wa kaskazini wa Dameski karibu na Hamathi utakuwa sehemu ya huo mpaka wake kuanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, haya ndiyo majina ya kabila hizo; toka mwisho wa pande za kaskazini, karibu na njia ya Hethloni, hata maingilio ya Hamathi, hata Hasar-enoni, penye mpaka wa Dameski, yaani, upande wa kaskazini karibu na Hamathi, watakuwa na upande wa mashariki, na upande wa magharibi; Dani fungu moja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: Kuanzia mpaka wa kaskazini kwenye barabara ya Hethloni hadi kuingia Hamathi hadi mji wa Hazar-enoni (ulioko mpakani mwa Damasko na Hamathi upande wa kaskazini na kuendelea kutoka mashariki hadi magharibi), eneo hilo litakuwa la kabila la Dani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: Kwenye mpaka wa kaskazini, Dani atakuwa na sehemu moja, mpaka huo utafuata barabara ya Hethloni hadi Lebo-Hamathi, Hasar-Enoni hata mpaka wa kaskazini wa Dameski karibu na Hamathi utakuwa sehemu ya huo mpaka wake kuanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: “Kwenye mpaka wa kaskazini, Dani atakuwa na sehemu moja, mpaka huo utafuata barabara ya Hethloni hadi Lebo-Hamathi, Hasar-Enani hata mpaka wa kaskazini wa Dameski karibu na Hamathi utakuwa sehemu ya huo mpaka wake kuanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, haya ndiyo majina ya makabila hayo; toka mwisho wa pande za kaskazini, karibu na njia ya Hethloni, hadi maingilio ya Hamathi, hadi Hasar-enoni, penye mpaka wa Dameski, yaani, upande wa kaskazini karibu na Hamathi, watakuwa na upande wa mashariki, na upande wa magharibi; Dani fungu moja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: Kuanzia mpaka wa kaskazini kwenye barabara ya Hethloni hadi kuingia Hamathi hadi mji wa Hazar-enoni (ulioko mpakani mwa Damasko na Hamathi upande wa kaskazini na kuendelea kutoka mashariki hadi magharibi), eneo hilo litakuwa la kabila la Dani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya ndiyo majina ya mashina: upande wa kaskazini kandokando ya njia ya Hetiloni kufika Hamati hata Hasari-Enani penye mpaka wa Damasko upande wa kaskazini kandokando ya Hamati ndiko kutakakokuwa fungu moja, la Dani toka upande wa maawioni kwa jua hata baharini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, haya ndiyo majina ya kabila hizo; toka mwisho wa pande za kaskazini, karibu na njia ya Hethloni, hata maingilio ya Hamathi, hata Hasar-enoni, penye mpaka wa Dameski, yaani, upande wa kaskazini karibu na Hamathi, watakuwa na upande wa mashariki, na upande wa magharibi; Dani fungu moja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: Kuanzia kwenye mupaka wa kaskazini kwenye barabara ya Hetiloni mpaka kuingia Hamati hata Hazorenoni unaokuwa katika Damasiki na Hamati upande wa kaskazini na kuendelea kutoka mashariki mpaka magaribi. Eneo hilo litakuwa la kabila la Dani.