Ezekiel 48:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makuhani watakuwa na eneo lao katika eneo hilo. Eneo hilo litakuwa na urefu wa kilomita kumi na mbili u nusu kutoka mashariki hadi magharibi, na kilomita 5 kutoka kaskazini hadi kusini. Maskani ya Mungu itakuwa katikati ya eneo hilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hii itakuwa ni sehemu takatifu kwa ajili ya makuhani. Itakuwa na urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano upande wa kaskazini, upana wa dhiraa elfu kumi upande wa magharibi, dhiraa elfu kumi upande wa mashariki, na urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano upande wa kusini. Katikati yake patakuwa mahali patakatifu pa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Matoleo hayo matakatifu yatakuwa kwa watu hawa, kwa makuhani; upande wa kaskazini urefu wake ishirini na tano elfu, na upande wa magharibi upana wake elfu kumi, na upande wa mashariki upana wake elfu kumi, na upande wa kusini urefu wake ishirini na tano elfu; na mahali patakatifu pa Bwana patakuwa katikati yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makuhani watakuwa na eneo lao katika eneo hilo. Eneo hilo litakuwa na urefu wa kilomita kumi na mbili u nusu kutoka mashariki hadi magharibi, na kilomita 5 kutoka kaskazini hadi kusini. Maskani ya Mungu itakuwa katikati ya eneo hilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hii itakuwa ni sehemu takatifu kwa ajili ya makuhani. Itakuwa na urefu wa dhiraa 25,000 upande wa kaskazini, upana wa dhiraa 10,000 upande wa magharibi, dhiraa 10,000 upande wa mashariki na urefu wa dhiraa 25,000 upande wa kusini. Katikati yake patakuwa mahali patakatifu pa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hii itakuwa ni sehemu takatifu kwa ajili ya makuhani. Itakuwa na urefu wa dhiraa 25,000 upande wa kaskazini, upana wa dhiraa 10,000 upande wa magharibi, dhiraa 10,000 upande wa mashariki na urefu wa dhiraa 25,000 upande wa kusini. Katikati yake patakuwa mahali patakatifu pa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Matoleo hayo matakatifu yatakuwa kwa ajili ya makuhani; upande wa kaskazini urefu wake mianzi elfu ishirini na tano, na upande wa magharibi upana wake mianzi elfu kumi, na upande wa mashariki upana wake mianzi elfu kumi, na upande wa kusini urefu wake mianzi elfu ishirini na tano; na mahali patakatifu pa BWANA patakuwa katikati yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makuhani watakuwa na eneo lao katika eneo hilo. Eneo hilo litakuwa na urefu wa kilomita kumi na mbili u nusu kutoka mashariki hadi magharibi, na kilomita 5 kutoka kaskazini hadi kusini. Maskani ya Mungu itakuwa katikati ya eneo hilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hilo fungu takatifu litakuwa lao watambikaji, wapate mahali penye kaskazini, urefu wake uwe mianzi 25000, nako upande wa baharini upana uwe mianzi 10000, nako upande wa maawioni kwa jua upana uwe mianzi 10000, tena kusini urefu uwe mianzi 25000, nako huko katikati kuwe na Patakatifu pa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Matoleo hayo matakatifu yatakuwa kwa watu hawa, kwa makuhani; upande wa kaskazini urefu wake ishirini na tano elfu, na upande wa magharibi upana wake elfu kumi, na upande wa mashariki upana wake elfu kumi, na upande wa kusini urefu wake ishirini na tano elfu; na mahali patakatifu pa BWANA patakuwa katikati yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Makuhani watakuwa na eneo lao katika eneo hilo. Eneo hilo litakuwa na urefu wa kilometre kumi na mbili na nusu kutoka mashariki mpaka magaribi, na kilometre tano kutoka kaskazini mpaka kusini. Hekalu la Mungu litakuwa katikati ya eneo hilo.