Ezekiel 48:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Eneo ambalo litabaki baada ya kujengwa hekalu, kusini mwa mji, kilomita 5 kwa kilomita 2.5, upande wa mashariki, na kilomita 5 kwa kilomita 2.5 upande wa magharibi, litakuwa eneo la wakulima kwa wakazi wa mji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Eneo linalobaki, linalopakana na sehemu takatifu likiwa na urefu sawa nalo, litakuwa dhiraa elfu kumi upande wa mashariki, na dhiraa elfu kumi upande wa magharibi. Mazao yake yatawapa watumishi wa mji chakula.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mabaki ya urefu wake yaelekeayo matoleo matakatifu, upande wa mashariki yatakuwa elfu kumi, na upande wa magharibi elfu kumi; nayo yatakuwa sawasawa na matoleo matakatifu; na mazao yake yatakuwa ni chakula cha watu wafanyao kazi humo mjini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Eneo ambalo litabaki baada ya kujengwa hekalu, kusini mwa mji, kilomita 5 kwa kilomita 2.5, upande wa mashariki, na kilomita 5 kwa kilomita 2.5 upande wa magharibi, litakuwa eneo la wakulima kwa wakazi wa mji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Eneo linalobaki, linalopakana na sehemu takatifu likiwa na urefu sawa nalo, litakuwa dhiraa 10,000 upande wa mashariki na dhiraa 10,000 upande wa magharibi. Mazao yake yatawapa watumishi wa mji chakula.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Eneo linalobaki, linalopakana na sehemu takatifu likiwa na urefu sawa nalo, litakuwa dhiraa 10,000 upande wa mashariki na dhiraa 10,000 upande wa magharibi. Mazao yake yatawapa watumishi wa mji chakula.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mabaki ya urefu wake yaelekeayo matoleo matakatifu, upande wa mashariki yatakuwa mianzi elfu kumi, na upande wa magharibi mianzi elfu kumi; nayo yatakuwa sawasawa na matoleo matakatifu; na mazao yake yatakuwa ni chakula cha watu wafanyao kazi humo mjini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Eneo ambalo litabaki baada ya kujengwa hekalu, kusini mwa mji, kilomita 5 kwa kilomita 2.5, upande wa mashariki, na kilomita 5 kwa kilomita 2.5 upande wa magharibi, litakuwa eneo la wakulima kwa wakazi wa mji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha patasalia kwa urefu kandokando ya lile fungu takatifu la kueuliwa mahali penye mianzi 10000 kuelekea maawioni kwa jua, na mianzi 10000 kuelekea baharini, ndipo kandokando ya lile fungu takatifu la kueuliwa; mahali hapo mazao yake yaliwe nao watumikiao mle mjini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mabaki ya urefu wake yaelekeayo matoleo matakatifu, upande wa mashariki yatakuwa elfu kumi, na upande wa magharibi elfu kumi; nayo yatakuwa sawasawa na matoleo matakatifu; na mazao yake yatakuwa ni chakula cha watu wafanyao kazi humo mjini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Eneo ambalo litabaki kisha kujengwa kwa hekalu, upande wa kusini wa muji, kilometre tano kwa kilometre mbili na nusu upande wa mashariki, na kilometre tano kwa kilometre mbili na nusu upande wa magaribi, litakuwa eneo la walimaji kwa wakaaji wa muji.