Ezekiel 48:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, eneo lote utakalotenga, yaani eneo takatifu pamoja na eneo la mji, litakuwa la mraba, kilomita kumi na mbili u nusu kila upande.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Eneo lote la hiyo sehemu litakuwa mraba, yaani dhiraa elfu ishirini na tano kila upande. Kama toleo maalum mtatenga sehemu takatifu, pamoja na milki ya mji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Matoleo yote yatakuwa ishirini na tano elfu, kwa ishirini na tano elfu; mtatoa matoleo matakatifu, nchi ya mraba, pamoja na milki ya mji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, eneo lote utakalotenga, yaani eneo takatifu pamoja na eneo la mji, litakuwa la mraba, kilomita kumi na mbili u nusu kila upande.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Eneo lote la hiyo sehemu litakuwa mraba, yaani, dhiraa 25,000 kila upande. Kama toleo maalum mtatenga sehemu takatifu, pamoja na milki ya mji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Eneo lote la hiyo sehemu litakuwa mraba, yaani, dhiraa 25,000 kila upande. Kama toleo maalum mtatenga sehemu takatifu, pamoja na milki ya mji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Matoleo yote yatakuwa mianzi elfu ishirini na tano, kwa mianzi elfu ishirini na tano; mtatoa matoleo matakatifu, nchi ya mraba, pamoja na milki ya mji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, eneo lote utakalotenga, yaani eneo takatifu pamoja na eneo la mji, litakuwa la mraba, kilomita kumi na mbili u nusu kila upande.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Fungu lote la kueuliwa, mtakalolitoa, liwe mianzi 25000 kwa pande zote nne, ndipo patakapokuwa fungu takatifu la kueuliwa pamoja na hilo fungu litakalokuwa lake huo mji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Matoleo yote yatakuwa ishirini na tano elfu, kwa ishirini na tano elfu; mtatoa matoleo matakatifu, nchi ya mraba, pamoja na milki ya mji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivyo, eneo lote utakalotenga, ni kusema eneo takatifu pamoja na eneo la muji litakuwa la muraba, kilometre kumi na mbili na nusu kila upande.