Ezekiel 48:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Eneo linalosalia katika pande zote za eneo takatifu na eneo la mji, yaani lile eneo lenye eneo mraba likiwa na kilomita kumi na mbili u nusus kwa kila upande tokea mashariki hadi magharibi, mkabala na maeneo ya makabila, litakuwa la mtawala. Lile eneo takatifu ambamo maskani ya Mungu itakuwa katikati yake,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Eneo linalobaki pande mbili za eneo linalofanya sehemu takatifu na milki ya mji litakuwa mali ya mkuu anayetawala. Eneo hili litaenea upande wa mashariki, kuanzia kwenye dhiraa elfu ishirini na tano za sehemu takatifu hadi mpaka wa mashariki, na kuelekea upande wa magharibi, kuanzia kwenye dhiraa elfu ishirini na tano hadi mpaka wa magharibi. Maeneo haya mawili yanayoenda sambamba na urefu wa sehemu za makabila yatakuwa ya mkuu anayetawala, na sehemu ile takatifu pamoja na mahali patakatifu pa Hekalu itakuwa katikati yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nayo mabaki yake yatakuwa ya huyo mkuu, upande huu na upande huu wa matoleo matakatifu, na milki ya mji, kuikabili hiyo ishirini na tano elfu ya matoleo, kuelekea mpaka wa mashariki; tena upande wa magharibi kuikabili hiyo ishirini na tano elfu, upande wa kuelekea mpaka wa magharibi; sawa na yale mafungu, hayo yatakuwa ya huyo mkuu; na matoleo matakatifu na mahali patakatifu pa nyumba patakuwa katikati yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Eneo linalosalia katika pande zote za eneo takatifu na eneo la mji, yaani lile eneo lenye eneo mraba likiwa na kilomita kumi na mbili u nusus kwa kila upande tokea mashariki hadi magharibi, mkabala na maeneo ya makabila, litakuwa la mtawala. Lile eneo takatifu ambamo maskani ya Mungu itakuwa katikati yake,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Eneo linalobaki pande zote za eneo linalofanya sehemu takatifu na milki ya mji litakuwa mali ya mkuu atawalaye. Eneo hili litaenea upande wa mashariki kuanzia kwenye dhiraa 25,000 za sehemu takatifu hadi mpaka wa mashariki na kuelekea upande wa magharibi kuanzia kwenye dhiraa 25,000 hadi mpaka wa magharibi. Maeneo yote haya mawili yanayoenda sambamba na urefu wa shemu za makabila yatakuwa ya mkuu anayetawala, na sehemu ile takatifu pamoja na mahali patakatifu pa Hekalu itakuwa katikati yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Eneo linalobaki pande zote za eneo linalofanya sehemu takatifu na milki ya mji litakuwa mali ya mkuu atawalaye. Eneo hili litaenea upande wa mashariki kuanzia kwenye dhiraa 25,000 za sehemu takatifu hadi mpaka wa mashariki na kuelekea upande wa magharibi kuanzia kwenye dhiraa 25,000 hadi mpaka wa magharibi. Maeneo yote haya mawili yanayoenda sambamba na urefu wa sehemu za makabila yatakuwa ya mkuu anayetawala, na sehemu ile takatifu pamoja na mahali patakatifu pa Hekalu itakuwa katikati yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nayo mabaki yake yatakuwa ya huyo mkuu, upande huu na upande huu wa matoleo matakatifu, na milki ya mji, kuikabili hiyo mianzi elfu ishirini na tano ya matoleo, kuelekea mpaka wa mashariki; tena upande wa magharibi kuikabili hiyo mianzi elfu ishirini na tano, upande wa kuelekea mpaka wa magharibi; sawa na yale mafungu, hayo yatakuwa ya huyo mkuu; na matoleo matakatifu na mahali patakatifu pa nyumba patakuwa katikati yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Eneo linalosalia katika pande zote za eneo takatifu na eneo la mji, yaani lile eneo lenye eneo mraba likiwa na kilomita kumi na mbili u nusus kwa kila upande tokea mashariki hadi magharibi, mkabala na maeneo ya makabila, litakuwa la mtawala. Lile eneo takatifu ambamo maskani ya Mungu itakuwa katikati yake,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Patakaposalia patakuwa pake mkuu upande wa huku na upande wa huko penye lile fungu takatifu la kueuliwa na penye lile fungu litakalokuwa lake huo mji kuifuata ile mianzi 25000 ya hilo fungu la kueuliwa mpakani kwenda upande wa maawioni kwa jua na upande wa baharini vilevile kuifuata ile mianzi 25000 kwenye mpaka uelekeao baharini sawasawa na mafungu mengine; hapo patakuwa pake mkuu. Hilo fungu takatifu la kueuliwa pamoja na Nyumba Takatifu itakuwa hapo katikati.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nayo mabaki yake yatakuwa ya huyo mkuu, upande huu na upande huu wa matoleo matakatifu, na milki ya mji, kuikabili hiyo ishirini na tano elfu ya matoleo, kuelekea mpaka wa mashariki; tena upande wa magharibi kuikabili hiyo ishirini na tano elfu, upande wa kuelekea mpaka wa magharibi; sawa na yale mafungu, hayo yatakuwa ya huyo mkuu; na matoleo matakatifu na mahali patakatifu pa nyumba patakuwa katikati yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Eneo linalobaki katika pande zote za eneo takatifu na eneo la muji, ni kusema lile eneo lenye eneo muraba likiwa na kilometre kumi na mbili na nusu kwa kila upande tokea mashariki mpaka magaribi, kuelekea maeneo ya makabila, litakuwa la mufalme. Lile eneo takatifu ambamo hekalu la Mungu litakuwa katikati yake,