Ezekiel 48:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya eneo la kabila la Yuda, utatenga eneo lenye urefu wa kilomita 12 na upana kama huohuo, kutoka kaskazini hadi kusini, na urefu huohuo kutoka mashariki hadi magharibi, sawasawa na eneo la kabila lolote. Hapo katikati ya eneo hilo patakuwa na maskani ya Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kupakana na nchi ya Yuda kuanzia mashariki mpaka magharibi itakuwa ndiyo sehemu utakayoitoa ili kuwa toleo maalum. Itakuwa na upana wa dhiraa elfu ishirini na tano, nao urefu wake kuanzia mashariki hadi magharibi utakuwa sawa na sehemu moja ya kabila; mahali patakatifu patakuwa katikati ya eneo hilo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mpakani mwa Yuda, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi, yatakuwapo matoleo mtakayotoa, upana wake mianzi ishirini na tano elfu, na urefu wake sawasawa na moja la mafungu hayo, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; na mahali patakatifu ni katikati yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya eneo la kabila la Yuda, utatenga eneo lenye urefu wa kilomita 12 na upana kama huohuo, kutoka kaskazini hadi kusini, na urefu huohuo kutoka mashariki hadi magharibi, sawasawa na eneo la kabila lolote. Hapo katikati ya eneo hilo patakuwa na maskani ya Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kupakana na nchi ya Yuda kuanzia mashariki mpaka magharibi itakuwa ndiyo sehemu utakayoitoa ili kuwa toleo maalum. Itakuwa na upana wa dhiraa 25,000 na urefu wake kuanzia mashariki mpaka magharibi utakuwa ule ule wa sehemu moja ya kabila, mahali patakatifu patakuwa katikati ya eneo hilo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kupakana na nchi ya Yuda kuanzia mashariki mpaka magharibi itakuwa ndiyo sehemu utakayoitoa ili kuwa toleo maalum. Itakuwa na upana wa dhiraa 25,000 na urefu wake kuanzia mashariki mpaka magharibi utakuwa ule ule wa sehemu moja ya kabila, mahali patakatifu patakuwa katikati ya eneo hilo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mpakani mwa Yuda, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi, yatakuwapo matoleo mtakayotoa, upana wake mianzi elfu ishirini na tano, na urefu wake sawasawa na moja la mafungu hayo, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; na mahali patakatifu ni katikati yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya eneo la kabila la Yuda, utatenga eneo lenye urefu wa kilomita 12 na upana kama huohuo, kutoka kaskazini hadi kusini, na urefu huohuo kutoka mashariki hadi magharibi, sawasawa na eneo la kabila lolote. Hapo katikati ya eneo hilo patakuwa na maskani ya Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwenye mpaka wa Yuda toka upande wa maawioni kwa jua hata upande wa baharini kuwe fungu la kueuliwa, mtakalolitoa; upana wake uwe mianzi 25000, tena urefu uwe kama fungu moja jingine toka upande wa maawioni kwa jua hata upande wa baharini; tena huko katikati kuwe na Patakatifu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mpakani mwa Yuda, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi, yatakuwapo matoleo mtakayotoa, upana wake mianzi ishirini na tano elfu, na urefu wake sawasawa na moja la mafungu hayo, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; na mahali patakatifu ni katikati yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha eneo la kabila la Yuda, utatenga eneo lenye urefu wa kilometre kumi na mbili na upana kama huohuo, kutoka kaskazini mpaka kusini, na urefu huohuo kutoka mashariki mpaka magaribi, sawasawa na eneo la kabila lolote. Hapo katikati ya eneo hilo patakuwa hekalu la Mungu.