Ezekiel 5:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu aliniambia, “Wewe mtu, jipatie upanga mkali, uutumie kama wembe wa kinyozi. Upitishe kichwani pako na kidevuni ili kunyoa nywele zako pamoja na ndevu zako. Kisha twaa mizani, uzipime nywele zako ili kuzigawanya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mwanadamu, chukua upanga mkali na uutumie kama wembe wa kinyozi ili kunyoa kichwa chako na ndevu zako. Kisha uchukue mizani, uzipime na kuzigawanya nywele hizo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe, mwanadamu, ujipatie upanga mkali, kama wembe wa kinyozi ujipatie, ukaupitishe juu ya kichwa chako na ndevu zako; kisha ujipatie mizani ya kupimia, ukazigawanye nywele hizo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu aliniambia, “Wewe mtu, jipatie upanga mkali, uutumie kama wembe wa kinyozi. Upitishe kichwani pako na kidevuni ili kunyoa nywele zako pamoja na ndevu zako. Kisha twaa mizani, uzipime nywele zako ili kuzigawanya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mwanadamu, sasa chukua upanga mkali na uutumie kama wembe wa kinyozi ili kunyolea nywele za kichwa chako na ndevu zako. Kisha uchukue mizani ya kupimia ukazigawanye nywele hizo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mwanadamu, sasa chukua upanga mkali na uutumie kama wembe wa kinyozi ili kunyolea nywele za kichwa chako na ndevu zako. Kisha uchukue mizani ya kupimia ukazigawanye nywele hizo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe, mwanadamu, ujipatie upanga mkali, kama wembe wa kinyozi ujipatie, ukaupitishe juu ya kichwa chako na ndevu zako; kisha ujipatie mizani ya kupimia, ukazigawanye nywele hizo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu aliniambia, “Wewe mtu, jipatie upanga mkali, uutumie kama wembe wa kinyozi. Upitishe kichwani pako na kidevuni ili kunyoa nywele zako pamoja na ndevu zako. Kisha twaa mizani, uzipime nywele zako ili kuzigawanya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe mwana wa mtu, jipatie upanga mkali, uutumie kuwa wembe wa kinyozi wa kunyolea kichwa chako na udevu wako! Kisha jipatie mizani, uzigawanye hizo nywele!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe, mwanadamu, ujipatie upanga mkali, kama wembe wa kinyozi ujipatie, ukaupitishe juu ya kichwa chako na ndevu zako; kisha ujipatie mizani ya kupimia, ukazigawanye nywele hizo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe aliniambia hivi: Wewe mwanadamu, utwae upanga mukali, uutumie kama wembe wa kinyozi. Unyoe kichwa na ndevu zako. Kisha utwae mizani, upime nywele zako na kuzigawanya kwa sehemu mbalimbali.