Ezekiel 5:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Theluthi moja ya watu wako, ee Yerusalemu, itakufa kwa maradhi mabaya na kwa njaa; theluthi nyingine itakufa vitani na theluthi inayobaki nitaitawanya pande zote za dunia na kuwafuatilia kwa upanga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Theluthi ya watu wako watakufa kwa tauni au kwa njaa humu ndani yako; theluthi nyingine itaanguka kwa upanga nje ya kuta zako; nayo theluthi nyingine nitaitawanya kwenye pande nne na kuwafuatia kwa upanga.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na kwa njaa watakomeshwa ndani yako; na theluthi yenu wataanguka kwa upanga pande zako zote; na theluthi yenu nitawatawanya kwa pepo zote, kisha nitafuta upanga nyuma yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Theluthi moja ya watu wako, ee Yerusalemu, itakufa kwa maradhi mabaya na kwa njaa; theluthi nyingine itakufa vitani na theluthi inayobaki nitaitawanya pande zote za dunia na kuwafuatilia kwa upanga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Theluthi ya watu wako watakufa kwa tauni au kwa njaa humu ndani yako, theluthi nyingine itaanguka kwa upanga nje ya kuta zako, nayo theluthi nyingine nitaitawanya kwenye pande nne kuwafuatia kwa upanga uliofutwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Theluthi ya watu wako watakufa kwa tauni au kwa njaa humu ndani yako, theluthi nyingine itaanguka kwa upanga nje ya kuta zako, nayo theluthi nyingine nitaitawanya kwenye pande nne kuwafuatia kwa upanga uliofutwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na kwa njaa watakomeshwa ndani yako; na theluthi yenu wataanguka kwa upanga pande zako zote; na theluthi yenu nitawatawanya kwa pepo zote, kisha nitafuta upanga nyuma yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Theluthi moja ya watu wako, ee Yerusalemu, itakufa kwa maradhi mabaya na kwa njaa; theluthi nyingine itakufa vitani na theluthi inayobaki nitaitawanya pande zote za dunia na kuwafuatilia kwa upanga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Fungu lako la tatu watakufa kwa magonjwa mabaya wakizimia kwa njaa katikati yako, fungu la tatu jingine watauawa kwa panga kwenye pande zako zote; fungu la tatu jingine nitawatupiatupia pande zote za upepo, kisha nitauchomoa upanga, uwafuate.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na kwa njaa watakomeshwa ndani yako; na theluthi yenu wataanguka kwa upanga pande zako zote; na theluthi yenu nitawatawanya kwa pepo zote, kisha nitafuta upanga nyuma yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sehemu moja ya tatu ya watu wako, ee Yerusalema, itakufa kwa ugonjwa mukali na kwa njaa. Sehemu ingine moja ya tatu itakufa katika vita. Na sehemu moja ya tatu inayobaki nitaisambaza pande zote za dunia na nitachomoa upanga wangu na kuwafuatilia nyuma.