Ezekiel 5:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ndivyo hasira yangu itakavyoishia, nami nitakuwa nimetuliza ghadhabu yangu na kuridhika moyoni. Hapo ndipo watakapojua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nimewaadhibu kwa kukosa uaminifu kwangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ndipo hasira yangu itakapokoma na ghadhabu yangu dhidi yao kupungua, nami nitakuwa nimejilipizia kisasi. Baada ya kuimaliza ghadhabu yangu juu yao, watajua kuwa Mimi, Mwenyezi Mungu, nimenena katika bidii yangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivyo ndivyo ghadhabu yangu itakavyotimia, nami nitatosheleza hasira yangu juu yao, nami nitafarijika; nao watajua ya kuwa mimi, Bwana, nimenena kwa wivu wangu, nitakapokuwa nimeitimiza ghadhabu yangu juu yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ndivyo hasira yangu itakavyoishia, nami nitakuwa nimetuliza ghadhabu yangu na kuridhika moyoni. Hapo ndipo watakapojua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nimewaadhibu kwa kukosa uaminifu kwangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ndipo hasira yangu itakapokoma na ghadhabu yangu dhidi yao itatulia, nami nitakuwa nimelipiza kisasi. Baada ya kuimaliza ghadhabu yangu juu yao, watajua kuwa mimi BWANA nimenena katika wivu wangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ndipo hasira yangu itakapokoma na ghadhabu yangu dhidi yao itatulia, nami nitakuwa nimelipiza kisasi. Baada ya kuimaliza ghadhabu yangu juu yao, watajua kuwa mimi bwana nimenena katika wivu wangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo ndivyo ghadhabu yangu itakavyotimia, nami nitatosheleza hasira yangu juu yao, nami nitafarijika; nao watajua ya kuwa mimi, BWANA, nimenena kwa wivu wangu, nitakapokuwa nimeitimiza ghadhabu yangu juu yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ndivyo hasira yangu itakavyoishia, nami nitakuwa nimetuliza ghadhabu yangu na kuridhika moyoni. Hapo ndipo watakapojua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nimewaadhibu kwa kukosa uaminifu kwangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo makali yangu yatakwisha, hivyo nitayapoza machafuko yangu yenye moto kwao nikiwalipisha. Ndipo, watakapotambua, ya kuwa mimi Bwana nimesema kwa wivu wangu, nikawatimilizia machafuko yangu yenye moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivyo ndivyo ghadhabu yangu itakavyotimia, nami nitatosheleza hasira yangu juu yao, nami nitafarijika; nao watajua ya kuwa mimi, BWANA, nimenena kwa wivu wangu, nitakapokuwa nimeitimiza ghadhabu yangu juu yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ndivyo nitakavyomaliza hasira yangu, nami nitakuwa nimetuliza kasirani yangu na kufarijika ndani ya moyo. Hapo ndipo watakapojua kwamba mimi, Yawe, nimewaazibu kwa sababu ya wivu wangu kwa ukosefu wenu wa uaminifu.