Ezekiel 5:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utakuwa kitu cha dharau na aibu, mfano wa kitu cha kuchukiza kwa makabila yanayokuzunguka, wakati nitakapotekeleza hukumu zangu dhidi yako kwa hasira na ghadhabu yangu kali. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Utakuwa kitu cha kudharauliwa na cha dhihaka, kitu cha onyo na cha kutisha kwa mataifa yanayokuzunguka, nitakapokupiga kwa adhabu katika hasira na ghadhabu yangu kwa kukukemea kwa ukali. Mimi Mwenyezi Mungu nimenena.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nayo itakuwa tukano na aibu, na mafundisho na ajabu, kwa mataifa wakuzungukao, hapo nitakapotekeleza hukumu ndani yako, kwa hasira, na kwa ghadhabu, na kwa malaumu ya ghadhabu; mimi, Bwana, nimeyanena hayo;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utakuwa kitu cha dharau na aibu, mfano wa kitu cha kuchukiza kwa makabila yanayokuzunguka, wakati nitakapotekeleza hukumu zangu dhidi yako kwa hasira na ghadhabu yangu kali. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Utakuwa kitu cha kudharauliwa na cha aibu, cha dhihaka, ovyo na kitu cha kutisha kwa mataifa yanayokuzunguka, nitakapokupiga kwa adhabu yangu katika hasira na ghadhabu yangu kwa kukukemea kwa ukali. Mimi BWANA nimesema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Utakuwa kitu cha kudharauliwa na cha aibu, cha dhihaka, ovyo na kitu cha kutisha kwa mataifa yanayokuzunguka, nitakapokupiga kwa adhabu yangu katika hasira na ghadhabu yangu kwa kukukemea kwa ukali. Mimi bwana nimesema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nayo itakuwa tukano na aibu, na mafundisho na ajabu, kwa mataifa wakuzungukao, hapo nitakapotekeleza hukumu ndani yako, kwa hasira, na kwa ghadhabu, na kwa adhabu kali; mimi, BWANA, nimeyanena hayo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utakuwa kitu cha dharau na aibu, mfano wa kitu cha kuchukiza kwa makabila yanayokuzunguka, wakati nitakapotekeleza hukumu zangu dhidi yako kwa hasira na ghadhabu yangu kali. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo itakuwa, uwe wa kuzomelewa na wa kufyozwa, tena uwe kitisho cha kuwashangaza wamizimu wakuzungukao, nitakapokufanyizia mashauri na kukutolea makali na machafuko yenye moto na mapigo yenye moto. Mimi Bwana nimeyasema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nayo itakuwa tukano na aibu, na mafundisho na ajabu, kwa mataifa wakuzungukao, hapo nitakapotekeleza hukumu ndani yako, kwa hasira, na kwa ghadhabu, na kwa malaumu ya ghadhabu; mimi, BWANA, nimeyanena hayo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utakuwa kitu cha kuzarauliwa na cha haya, mufano wa kitu cha kuchukiza kwa makabila yanayokuzunguka, wakati nitakapotimiza hukumu zangu juu yako kwa hasira na kasirani yangu kali. Ni mimi Yawe ninayasema hivyo.