Ezekiel 5:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo nitaiachilia mishale yangu mikali ya njaa iwachome na kuangamiza wakazi wako. Nitawafanya wafe njaa kwa kuiharibu akiba yao ya chakula.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitakapokurushia mishale yangu ya kufisha na yenye kuharibu ya njaa, nitairusha ili kukuangamiza. Nitaleta njaa zaidi na zaidi juu yako na kukomesha upatikanaji wa chakula kwako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hapo nitakapopeleka mishale mibaya ya njaa juu yao, iletayo uharibifu, nitakayoipeleka ili kuwaharibu ninyi; nami nitaiongeza njaa juu yenu, na tegemeo lenu la mkate nitalivunja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo nitaiachilia mishale yangu mikali ya njaa iwachome na kuangamiza wakazi wako. Nitawafanya wafe njaa kwa kuiharibu akiba yao ya chakula.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitakapokupiga kwa mishale yangu ya kufisha na yenye kuharibu ya njaa, nitaipiga ili kukuangamiza. Nitaleta njaa zaidi na zaidi juu yako na kukomesha upatikanaji kwako wa chakula.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitakapokupiga kwa mishale yangu ya kufisha na yenye kuharibu ya njaa, nitaipiga ili kukuangamiza. Nitaleta njaa zaidi na zaidi juu yako na kukomesha upatikanaji wa chakula kwako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hapo nitakapoiachilia mishale mibaya ya njaa juu yao, mishale iletayo uharibifu nitakayoiachilia ili kuwaharibu ninyi; nami nitaiongeza njaa juu yenu, na tegemeo lenu la mkate nitalivunja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo nitaiachilia mishale yangu mikali ya njaa iwachome na kuangamiza wakazi wako. Nitawafanya wafe njaa kwa kuiharibu akiba yao ya chakula.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, nitakapowapigia mishale mibaya ya njaa ya kuangamiza; hiyo ndiyo, nitakayoipiga kweli, iwaangamize ninyi, nitakapoizidisha njaa na kulivunja kabis shikizo lenu la chakula.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hapo nitakapopeleka mishale mibaya ya njaa juu yao, iletayo uharibifu, nitakayoipeleka ili kuwaharibu ninyi; nami nitaiongeza njaa juu yenu, na tegemeo lenu la mkate nitalivunja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati huo nitaiachilia mishale yangu mikali ya njaa iwachome na kuangamiza wakaaji wako. Nitawafanya wakufe na njaa kwa kuiharibu akiba yao ya chakula.