Ezekiel 5:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitakupelekea njaa na wanyama wakali ambao watakupokonya watoto wako; maradhi mabaya, mauaji, na vita vitakuja kukuangamiza. Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitatuma njaa na wanyama pori dhidi yako, navyo vitakuacha bila watoto. Tauni na umwagaji wa damu vitapita katikati yako, nami nitaleta upanga juu yako. Mimi Mwenyezi Mungu nimenena.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitapeleka juu yenu njaa na wanyama wabaya, nao watakunyang'anya watu wako; na tauni na damu zitapita ndani yako; nami nitauleta upanga juu yako; mimi Bwana, nimeyanena hayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitakupelekea njaa na wanyama wakali ambao watakupokonya watoto wako; maradhi mabaya, mauaji, na vita vitakuja kukuangamiza. Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitapeleka njaa na wanyama wa mwituni dhidi yenu, navyo vitawaacha bila watoto. Tauni na umwagaji wa damu utapita katikati yenu, nami nitaleta upanga juu yenu. Mimi BWANA nimenena haya.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitapeleka njaa na wanyama wa mwituni dhidi yenu, navyo vitawaacha bila watoto. Tauni na umwagaji wa damu utapita katikati yenu, nami nitaleta upanga juu yenu. Mimi bwana nimenena haya.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitatuma njaa na wanyama wabaya juu yenu, nao watakunyang'anya watu wako; na tauni na damu zitapita ndani yako; nami nitauleta upanga juu yako; mimi BWANA, nimeyanena hayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitakupelekea njaa na wanyama wakali ambao watakupokonya watoto wako; maradhi mabaya, mauaji, na vita vitakuja kukuangamiza. Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pamoja na hiyo njaa nitawapelekea nyama wabaya, wawaue watoto wako, nayo magonjwa mabaya ya kuozesha damu yatapita kwako, kisha nitaleta nazo panga na kukuua. Mimi Bwana nimeyasema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitapeleka juu yenu njaa na wanyama wabaya, nao watakunyang’anya watu wako; na tauni na damu zitapita ndani yako; nami nitauleta upanga juu yako; mimi BWANA, nimeyanena hayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitakutumia njaa na nyama wakali ambao wataua watoto wako; magonjwa makali, mauaji, na vita itakuja kukuangamiza. Ni mimi, Yawe, ninayesema hivyo.