Ezekiel 5:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya kuzingirwa kwa mji wa Yerusalemu kumalizika, utaichoma theluthi ya nywele zako ndani ya mji. Theluthi nyingine utaipigapiga kwa upanga ukiuzunguka mji. Theluthi ya mwisho utaitawanya kwa upepo, nami nitauchomoa upanga wangu ili kuifuatilia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku zako za kuzingirwa zitakapokwisha, choma theluthi moja ya nywele ndani ya mji. Chukua theluthi nyingine ya hizo nywele uzikatekate kwa upanga ukiuzunguka mji wote, na theluthi ya mwisho uitawanye kwa upepo, kwa kuwa nitawafuatia kwa upanga uliovutwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Theluthi ya hizo utaiteketeza katikati ya mji, siku za mazingiwa zitakapotimia; nawe utatwaa theluthi, na kuipiga kwa upanga pande zote; nawe utatawanya theluthi ichukuliwe na upepo, nami nitafuta upanga nyuma yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya kuzingirwa kwa mji wa Yerusalemu kumalizika, utaichoma theluthi ya nywele zako ndani ya mji. Theluthi nyingine utaipigapiga kwa upanga ukiuzunguka mji. Theluthi ya mwisho utaitawanya kwa upepo, nami nitauchomoa upanga wangu ili kuifuatilia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati siku zako za kuzingirwa zitakapokwisha, choma theluthi moja ya hizo nywele zako kwa moto ndani ya mji. Chukua theluthi nyingine ya hizo nywele uzipige kwa upanga kuuzunguka mji wote na theluthi nyingine ya mwisho utaitawanya kwa upepo. Kwa kuwa nitawafuatia kwa upanga uliofutwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati siku zako za kuzingirwa zitakapokwisha, choma theluthi moja ya hizo nywele zako kwa moto ndani ya mji. Chukua theluthi nyingine ya hizo nywele uzipige kwa upanga kuuzunguka mji wote na theluthi nyingine ya mwisho utaitawanya kwa upepo. Kwa kuwa nitawafuatia kwa upanga uliofutwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Theluthi ya hizo utaiteketeza katikati ya mji, siku za kuzingirwa zitakapomalizika; nawe utatwaa theluthi, na kuipiga kwa upanga pande zote; nawe utatawanya theluthi ichukuliwe na upepo, nami nitafuta upanga nyuma yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya kuzingirwa kwa mji wa Yerusalemu kumalizika, utaichoma theluthi ya nywele zako ndani ya mji. Theluthi nyingine utaipigapiga kwa upanga ukiuzunguka mji. Theluthi ya mwisho utaitawanya kwa upepo, nami nitauchomoa upanga wangu ili kuifuatilia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Fungu la tatu uliteketeze kwa moto mjini katikati, siku za kusongwa zitakapomalizika! Fungu la tatu jingine lichukue, ulitapanye na kupigapiga kwa upanga ukizunguka mjini po pote! Nalo fungu la tatu jingine utalitupatupa kwenye upepo, nami nitauchomoa upanga, uzifuata nyuma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Theluthi ya hizo utaiteketeza katikati ya mji, siku za mazingiwa zitakapotimia; nawe utatwaa theluthi, na kuipiga kwa upanga pande zote; nawe utatawanya theluthi ichukuliwe na upepo, nami nitafuta upanga nyuma yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha kutimia kwa wakati wa kushambuliwa kwa muji wa Yerusalema, utachoma sehemu moja ya tatu ya nywele zako katikati ya muji. Sehemu ingine moja ya tatu utaikatakata kwa upanga ukiuzunguka muji. Sehemu ya tatu ya mwisho utaipeperusha kwa upepo, nami nitauchomoa upanga wangu na kuwafuatilia nyuma.