Ezekiel 5:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kwa kuwa nyinyi ni wakaidi kuliko mataifa yanayowazunguka, kwa kuwa hamkuishi kulingana na kanuni zangu, wala hamkuyashika maagizo yangu, ila mmetenda kulingana na maagizo ya mataifa yanayowazunguka,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ninyi mmekuwa wakaidi kuliko mataifa yanayowazunguka na hamkufuata maagizo yangu wala kuzishika sheria zangu. Wala hamkuweza hata kuzifuata desturi za mataifa yanayowazunguka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, kwa hiyo Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu ninyi mmefanya ghasia kuliko mataifa wawazungukao ninyi, wala hamkuenda katika sheria zangu, wala hamkuzishika hukumu zangu, wala hamkutenda kama kawaida za mataifa wawazungukao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kwa kuwa nyinyi ni wakaidi kuliko mataifa yanayowazunguka, kwa kuwa hamkuishi kulingana na kanuni zangu, wala hamkuyashika maagizo yangu, ila mmetenda kulingana na maagizo ya mataifa yanayowazunguka,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa hiyo hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Ninyi mmekuwa wakaidi kuliko mataifa yanayowazunguka na hamkufuata amri zangu wala kuzishika sheria zangu. Wala hamkuweza hata kuzifuata kawaida za mataifa yanayowazunguka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa hiyo hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Ninyi mmekuwa wakaidi kuliko mataifa yanayowazunguka na hamkufuata amri zangu wala kuzishika sheria zangu. Wala hamkuweza hata kuzifuata kawaida za mataifa yanayowazunguka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, kwa hiyo Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu ninyi mmefanya ghasia kuliko mataifa wawazungukao ninyi, wala hamkuenda katika sheria zangu, wala hamkuzishika amri zangu, wala hamkutenda kama kawaida za mataifa wawazungukao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kwa kuwa nyinyi ni wakaidi kuliko mataifa yanayowazunguka, kwa kuwa hamkuishi kulingana na kanuni zangu, wala hamkuyashika maagizo yangu, ila mmetenda kulingana na maagizo ya mataifa yanayowazunguka,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu hii Bwana Mungu anasema hivi: Kwa kuwa mnafanya matata kuliko wamizimu wanaowazunguka, msipoyafuata maongozi yangu, wala msipoyafanya mashauri yangu, wala msipoyafanya maamuzi yangu, wamizimu wawazungukao wanayoyafanya,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, kwa hiyo Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu ninyi mmefanya ghasia kuliko mataifa wawazungukao ninyi, wala hamkuenda katika sheria zangu, wala hamkuzishika hukumu zangu, wala hamkutenda kama kawaida za mataifa wawazungukao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, Bwana wetu Yawe anasema hivi: Ninyi ni waasi kuliko mataifa yanayowazunguka, hamukuishi kulingana na masharti yangu, wala hamukuyashika maagizo yangu, lakini mumetenda kulingana na maagizo ya mataifa yanayowazunguka.