Ezekiel 6:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitaunyosha mkono wangu dhidi yao, na kuiharibu nchi yao. Tangu huko jangwani kusini mpaka mjini Ribla kaskazini, nitaifanya nchi yao kuwa mahame kabisa wasipate mahali pa kuishi. Hapo ndipo wote watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nami nitanyoosha mkono wangu dhidi yao na kuifanya nchi yao ukiwa, kuanzia jangwani hadi Dibla, kila mahali wanapoishi. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitanyosha mkono wangu juu yao, na kuifanya nchi kuwa maganjo, tena ukiwa mbaya kuliko jangwa upande wa Dibla, katika makao yao yote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitaunyosha mkono wangu dhidi yao, na kuiharibu nchi yao. Tangu huko jangwani kusini mpaka mjini Ribla kaskazini, nitaifanya nchi yao kuwa mahame kabisa wasipate mahali pa kuishi. Hapo ndipo wote watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nami nitanyosha mkono wangu dhidi yao na kuifanya nchi yao ukiwa, kuanzia jangwani hadi Dibla, kila mahali po pote wanapoishi. Ndipo watakapojua ya kwamba Mimi ndimi BWANA.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nami nitanyoosha mkono wangu dhidi yao na kuifanya nchi yao ukiwa, kuanzia jangwani hadi Dibla, kila mahali wanapoishi. Ndipo watakapojua ya kwamba Mimi ndimi bwana.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitanyosha mkono wangu juu yao, na kuifanya nchi kuwa maganjo, tena ukiwa mbaya kuliko jangwa upande wa Dibla, katika makao yao yote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitaunyosha mkono wangu dhidi yao, na kuiharibu nchi yao. Tangu huko jangwani kusini mpaka mjini Ribla kaskazini, nitaifanya nchi yao kuwa mahame kabisa wasipate mahali pa kuishi. Hapo ndipo wote watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitawakunjulia mkono wangu, nchi hii niigeuze kuwa mapori yaliyo peke yao kuanzia kwenye nyika kufikisha kwenye Dibula po pote, wanapokaa; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitanyosha mkono wangu juu yao, na kuifanya nchi kuwa maganjo, tena ukiwa mbaya kuliko jangwa upande wa Dibla, katika makao yao yote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitanyoosha mukono wangu juu yao, na kuiharibu inchi yao. Tangu huko katika jangwa upande wa kusini mpaka katika muji wa Dibla kwa upande wa kaskazini, nitaifanya inchi yao kuwa matongo kabisa wasipate pahali pa kuishi. Nao watatambua kwamba mimi ni Yawe.