Ezekiel 6:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na kusema: Sikilizeni neno la Bwana Mwenyezi-Mungu enyi wakazi wa milima ya Israeli: Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nawaambieni nyinyi wakazi wa milimani na vilimani, wa magengeni na mabondeni kwamba mimi mwenyewe nitaleta upanga na kuharibu sehemu zenu zote zilizoinuka za ibada.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
useme, ‘Ee milima ya Israeli, sikieni neno la Bwana Mungu Mwenyezi. Hili ndilo neno asemalo Bwana Mungu Mwenyezi kwa milima na vilima, magenge na mabonde: Nakaribia kuleta upanga dhidi yenu, na nitapaharibu mahali penu pa juu pa kuabudia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ukisema, Enyi milima ya Israeli, lisikieni neno la Bwana MUNGU; Bwana MUNGU aiambia hivi milima na vilima, na vijito na mabonde; Tazama, mimi, naam, mimi, nitaleta upanga juu yenu, nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na kusema: Sikilizeni neno la Bwana Mwenyezi-Mungu enyi wakazi wa milima ya Israeli: Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nawaambieni nyinyi wakazi wa milimani na vilimani, wa magengeni na mabondeni kwamba mimi mwenyewe nitaleta upanga na kuharibu sehemu zenu zote zilizoinuka za ibada.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na useme: ‘Ee milima ya Israeli, sikia neno la BWANA Mwenyezi. Hili ndilo BWANA Mwenyezi aliambiayo milima na vilima, magenge na mabonde: Ninakaribia kuleta upanga dhidi yenu, nami nitapaharibu mahali penu pote pa juu pa kuabudia miungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na useme: ‘Ee milima ya Israeli, sikia neno la bwana Mwenyezi. Hili ndilo bwana Mwenyezi aliambiayo milima na vilima, magenge na mabonde: Ninakaribia kuleta upanga dhidi yenu, nami nitapaharibu mahali penu pote pa juu pa kuabudia miungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ukisema, Enyi milima ya Israeli, lisikieni neno la Bwana MUNGU; Bwana MUNGU aiambia hivi milima na vilima, na vijito na mabonde; Tazama, mimi, naam, mimi, nitaleta upanga juu yenu, nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na kusema: Sikilizeni neno la Bwana Mwenyezi-Mungu enyi wakazi wa milima ya Israeli: Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nawaambieni nyinyi wakazi wa milimani na vilimani, wa magengeni na mabondeni kwamba mimi mwenyewe nitaleta upanga na kuharibu sehemu zenu zote zilizoinuka za ibada.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Useme: Milima ya Isiraeli, lisikieni neno la Bwana Mungu! Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema, mvisikie ninyi milima na vilima na vijito na mabonde: Mtaniona, nikileta panga kwenu, niyakomeshe matambiko yenu ya vilimani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ukisema, Enyi milima ya Israeli, lisikieni neno la Bwana MUNGU; Bwana MUNGU aiambia hivi milima na vilima, na vijito na mabonde; Tazama, mimi, naam, mimi, nitaleta upanga juu yenu, nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na kusema hivi: Musikilize neno la Bwana wetu Yawe, enyi wakaaji wa milima ya Israeli! Anawaambia ninyi wakaaji wenye kuwa katika milima na vilima na katika maporomoko na mabonde kwamba: Mimi mwenyewe, Bwana wenu Yawe, nitaleta upanga na kuharibu sehemu zenu zote zilizoinuka za kutambikia.