Ezekiel 7:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watavaa mavazi ya gunia, hofu itawashika, nao watakuwa na aibu, vichwa vyao vyote vitanyolewa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watavaa gunia na kufunikwa na hofu. Nyuso zao zitafunikwa na aibu, na vichwa vyao vitanyolewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena watajifungia nguo za magunia, na utisho utawafunika; na aibu itakuwa juu ya nyuso zote, na upaa juu ya vichwa vyao vyote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watavaa mavazi ya gunia, hofu itawashika, nao watakuwa na aibu, vichwa vyao vyote vitanyolewa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watavaa nguo ya gunia na kufunikwa na hofu. Nyuso zao zitafunikwa na aibu na nywele za vichwa vyao zitanyolewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watavaa nguo ya gunia na kufunikwa na hofu. Nyuso zao zitafunikwa na aibu na nywele za vichwa vyao zitanyolewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena watajifungia nguo za magunia, na utisho utawafunika; na aibu itakuwa juu ya nyuso zote, na upaa juu ya vichwa vyao vyote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watavaa mavazi ya gunia, hofu itawashika, nao watakuwa na aibu, vichwa vyao vyote vitanyolewa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watajifunga magunia, wakipigwa na bumbuazi sana, nyuso zao zote, zitaiva kwa kuona soni, navyo vichwa vyao vyote vitakuwa vimenyolewa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena watajifungia nguo za magunia, na utisho utawafunika; na aibu itakuwa juu ya nyuso zote, na upaa juu ya vichwa vyao vyote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watavaa gunia, hofu itawashika, nao watapata haya na vichwa vyao vyote vitanyolewa.