Ezekiel 7:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watatupa fedha yao barabarani na dhahabu yao itakuwa kama kitu najisi. Fedha na dhahabu zao hazitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu; wala hawataweza kushiba au kuyajaza matumbo yao fedha na dhahabu waliyojirundikia; kwani mali hiyo ndiyo chanzo cha dhambi yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Watatupa fedha yao barabarani, nayo dhahabu yao itakuwa najisi. Fedha yao na dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Hawatashibisha njaa yao au kujaza tumbo zao kwa hiyo fedha wala dhahabu, kwa sababu imewaponza wajikwae dhambini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watatupa fedha yao katika njia kuu za mji, na dhahabu yao itakuwa kama kitu cha unajisi; fedha yao na dhahabu yao hazitaweza kuwaokoa siku ya ghadhabu ya Bwana; hawatajishibisha roho zao, wala hawatajijaza matumbo yao; kwa sababu zilikuwa kwazo la uovu wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watatupa fedha yao barabarani na dhahabu yao itakuwa kama kitu najisi. Fedha na dhahabu zao hazitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu; wala hawataweza kushiba au kuyajaza matumbo yao fedha na dhahabu waliyojirundikia; kwani mali hiyo ndiyo chanzo cha dhambi yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watatupa fedha yao barabarani, nayo dhahabu yao itakuwa najisi. Fedha yao na dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya BWANA. Hawatashibisha njaa yao au kujaza matumbo yao kwa hiyo fedha wala dhahabu, kwa sababu imewaponza wajikwae dhambini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watatupa fedha yao barabarani, nayo dhahabu yao itakuwa najisi. Fedha yao na dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya bwana. Hawatashibisha njaa yao au kujaza matumbo yao kwa hiyo fedha wala dhahabu, kwa sababu imewaponza wajikwae dhambini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watatupa fedha yao katika njia kuu za mji, na dhahabu yao itakuwa kama kitu cha unajisi; fedha yao na dhahabu yao hazitaweza kuwaokoa siku ya ghadhabu ya BWANA; hawatajishibisha roho zao, wala hawatajijaza matumbo yao; kwa sababu zilikuwa kwazo la uovu wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watatupa fedha yao barabarani na dhahabu yao itakuwa kama kitu najisi. Fedha na dhahabu zao hazitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu; wala hawataweza kushiba au kuyajaza matumbo yao fedha na dhahabu waliyojirundikia; kwani mali hiyo ndiyo chanzo cha dhambi yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Fedha zao watazitupa barabarani, nazo dhahabu zao zitakuwa kama zenye uchafu, kwani dhahabu zao na fedha zao hazitaweza kuwaponya siku hiyo, Bwana atakapochafuka, wala hazitazishibisha roho zao, wala hazitayajaza matumbo yao, kwani ndizo zilizowaponza, wazikore manza zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watatupa fedha yao katika njia kuu za mji, na dhahabu yao itakuwa kama kitu cha unajisi; fedha yao na dhahabu yao hazitaweza kuwaokoa siku ya ghadhabu ya BWANA; hawatajishibisha roho zao, wala hawatajijaza matumbo yao; kwa sababu zilikuwa kwazo la uovu wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watatupa feza yao ndani ya barabara na zahabu yao itakuwa kama kitu kichafu. Feza na zahabu zao hazitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya kasirani ya Yawe; wala hawataweza kushiba au kujaza tumbo zao feza na zahabu waliyojilundikia; maana mali hiyo ndiyo iliyosababisha zambi yao.