Ezekiel 7:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme ataomboleza, mkuu atakata tamaa na watu watatetemeka kwa hofu. Nitawatenda kadiri ya mienendo yao, nitawahukumu kama nilivyowahukumu wengine. Ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme ataomboleza, mwana wa mfalme atavikwa kukata tamaa, nayo mikono ya watu wa nchi itatetemeka. Nitawaadhibu kulingana na matendo yao, na kwa kanuni zao wenyewe nitawahukumu. “ ‘Ndipo watajua kwamba Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme ataomboleza, na mkuu atavikwa ukiwa, na mikono ya watu wa nchi itataabika; nitawatenda sawasawa na njia yao; nami nitawahukumu sawasawa na kustahili kwao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme ataomboleza, mkuu atakata tamaa na watu watatetemeka kwa hofu. Nitawatenda kadiri ya mienendo yao, nitawahukumu kama nilivyowahukumu wengine. Ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme ataomboleza, mwana wa mfalme atavikwa kukata tamaa, nayo mikono ya watu wa nchi itatetemeka. Nitawashughulikia sawasawa na matendo yao na kwa kanuni zao wenyewe nitawahukumu. Ndipo watajua kwamba Mimi ndimi BWANA.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme ataomboleza, mwana wa mfalme atavikwa kukata tamaa, nayo mikono ya watu wa nchi itatetemeka. Nitawashughulikia sawasawa na matendo yao na kwa kanuni zao wenyewe nitawahukumu. Ndipo watajua kwamba Mimi ndimi bwana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme ataomboleza, na mkuu atavikwa ukiwa, na mikono ya watu wa nchi itataabika; nitawatenda kulingana na njia yao; nami nitawahukumu kulingana na kustahili kwao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme ataomboleza, mkuu atakata tamaa na watu watatetemeka kwa hofu. Nitawatenda kadiri ya mienendo yao, nitawahukumu kama nilivyowahukumu wengine. Ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme ataomboleza, naye aliye mkuu kituko kitakuwa vazi lake, nayo mikono ya watu wa nchi hii itastushwa; nitakapowalipisha njia zao na kuwakatia shauri liyapasalo mashauri yao, ndipo watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme ataomboleza, na mkuu atavikwa ukiwa, na mikono ya watu wa nchi itataabika; nitawatenda sawasawa na njia yao; nami nitawahukumu sawasawa na kustahili kwao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme ataomboleza, mukubwa atakata tamaa na watu watatetemeka kwa hofu. Nitawatendea kufuatana na mienendo yao, nitawahukumu kama nilivyowahukumu wengine. Halafu watatambua kwamba mimi ni Yawe.