Ezekiel 7:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sitawaachia wala sitawahurumia; nitawaadhibu kulingana na mienendo yenu, maadamu machukizo bado yapo kati yenu. Ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sitawaonea huruma wala kuwarehemu. Hakika nitawalipiza kwa ajili ya matendo yenu na desturi za machukizo miongoni mwenu. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jicho langu halitakuachilia, wala sitaona huruma; bali nitakupatiliza njia zako, na machukizo yako yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sitawaachia wala sitawahurumia; nitawaadhibu kulingana na mienendo yenu, maadamu machukizo bado yapo kati yenu. Ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sitawaonea huruma wala sitawarehemu, hakika nitapiza kwa ajili ya matendo yenu na desturi zenu za machukizo miongoni mwenu. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sitawaonea huruma wala sitawarehemu, hakika nitalipiza kwa ajili ya matendo yenu na desturi zenu za machukizo miongoni mwenu. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jicho langu halitakuachilia, wala sitaona huruma; bali nitakupatiliza njia zako, na machukizo yako yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sitawaachia wala sitawahurumia; nitawaadhibu kulingana na mienendo yenu, maadamu machukizo bado yapo kati yenu. Ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jicho langu halitakuonea uchungu, wala mimi sitakuhurumia, kwani nitakulipisha njia zako, machukizo yako yatokee kwako katikati; ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jicho langu halitakuachilia, wala sitaona huruma; bali nitakupatiliza njia zako, na machukizo yako yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sitawaachilia wala sitawaonea huruma. Nitawaazibu kulingana na mienendo yenu, nayo machukizo yenu yangali bado kati yenu. Halafu mutatambua kwamba mimi ni Yawe.