Ezekiel 7:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sitawaachilia wala sitawaonea huruma. Nitawaadhibu kulingana na mienendo yenu maadamu machukizo yapo bado miongoni mwenu. Ndipo mtakapotambua kuwa ni mimi Mwenyezi-Mungu ninayewaangamiza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sitawaonea huruma wala kuwarehemu. Nitawalipiza kwa ajili ya matendo yenu na desturi za machukizo miongoni mwenu. “ ‘Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu ambaye huwapiga.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; nitakupatiliza njia zako na machukizo yako yote yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, napiga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sitawaachilia wala sitawaonea huruma. Nitawaadhibu kulingana na mienendo yenu maadamu machukizo yapo bado miongoni mwenu. Ndipo mtakapotambua kuwa ni mimi Mwenyezi-Mungu ninayewaangamiza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sitawaonea huruma wala sitawarehemu; nitawalipiza sawasawa na matendo yenu na desturi zenu za machukizo miongoni mwenu. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi BWANA ambaye huwapiga kwa mapigo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sitawaonea huruma wala sitawarehemu; nitawalipiza sawasawa na matendo yenu na desturi zenu za machukizo miongoni mwenu. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi bwana ambaye huwapiga kwa mapigo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; nitakupatiliza njia zako na machukizo yako yote yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi, BWANA, napiga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sitawaachilia wala sitawaonea huruma. Nitawaadhibu kulingana na mienendo yenu maadamu machukizo yapo bado miongoni mwenu. Ndipo mtakapotambua kuwa ni mimi Mwenyezi-Mungu ninayewaangamiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jicho langu halitokuonea uchungu, wala mimi sitakuhurumia nikikulipisha njia zako, machukizo yako yatokee kwako katikati; ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana apigaye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; nitakupatiliza njia zako na machukizo yako yote yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi, BWANA, napiga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sitawaachilia wala sitawaonea huruma. Nitawaazibu kulingana na mienendo yenu nayo machukizo yangali bado kati yenu. Halafu mutatambua kwamba ni mimi Yawe ninayewaangamiza.