Ezekiel 8:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akanichukua mpaka lango la kaskazini la nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Huko kulikuwa na wanawake wameketi wakimwombolezea Tamuzi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo akanileta kwenye ingilio la lango la kaskazini la nyumba ya Mwenyezi Mungu, nami nikaona wanawake wameketi hapo, wakimwombolezea Tamuzi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo akanileta mpaka mlango wa kuingilia katika nyumba ya Bwana, ulioelekea upande wa kaskazini, na tazama, wanawake wameketi wakimlilia Tamuzi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akanichukua mpaka lango la kaskazini la nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Huko kulikuwa na wanawake wameketi wakimwombolezea Tamuzi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo akanileta mpaka ingilio la lango la kaskazini la nyumba ya BWANA, nami nikaona wanawake wameketi hapo, wakimwombolezea Tamuzi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo akanileta mpaka ingilio la lango la kaskazini la nyumba ya bwana, nami nikaona wanawake wameketi hapo, wakimwombolezea Tamuzi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo akanileta mpaka maingilio ya lango la kaskazini mwa nyumba ya BWANA, ulioelekea upande wa kaskazini, na tazama, wanawake wameketi wakimlilia Tamuzi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akanichukua mpaka lango la kaskazini la nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Huko kulikuwa na wanawake wameketi wakimwombolezea Tamuzi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akanipeleka penye lango la kuingia Nyumbani mwa Bwana lililoko upande wa kaskazini, nikaona humo wanawake waliokaa wakimlilia Tamuzi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo akanileta mpaka mlango wa kuingilia katika nyumba ya BWANA, ulioelekea upande wa kaskazini, na tazama, wanawake wameketi wakimlilia Tamuzi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akanipeleka mpaka kwenye mulango wa upande wa kaskazini wa nyumba ya Yawe. Huko kulikuwa wanawake wameikaa wakimwombolezea mungu Tamuzi.