Ezekiel 8:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akanipeleka mpaka ua wa ndani ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Huko mlangoni mwa hekalu, kati ya ukumbi na madhabahu, walikuwapo wanaume wapatao ishirini na watano, wakilipa kisogo hekalu, na nyuso zao zimeelekea upande wa mashariki. Walikuwa wanaabudu jua wakielekea upande wa mashariki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo akanileta hadi kwenye ukumbi wa ndani wa nyumba ya Mwenyezi Mungu, na katika ingilio la Hekalu, kati ya baraza na madhabahu, palikuwa na wanaume wapatao ishirini na watano. Walikuwa wamelipa kisogo Hekalu la Mwenyezi Mungu na kuelekeza nyuso zao upande wa mashariki, wakilisujudia jua upande wa mashariki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akanileta mpaka ua wa ndani wa nyumba ya Bwana, na tazama, mlangoni pa hekalu la Bwana, kati ya ukumbi na madhabahu, walikuwako watu kama ishirini na watano, wamelipa kisogo hekalu la Bwana, na nyuso zao zimeelekea upande wa mashariki, nao wanaliabudu jua, kwa kuuelekea upande wa mashariki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akanipeleka mpaka ua wa ndani ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Huko mlangoni mwa hekalu, kati ya ukumbi na madhabahu, walikuwapo wanaume wapatao ishirini na watano, wakilipa kisogo hekalu, na nyuso zao zimeelekea upande wa mashariki. Walikuwa wanaabudu jua wakielekea upande wa mashariki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo akanileta mpaka kwenye ukumbi wa ndani wa nyumba ya BWANA, nako huko katika ingilio la Hekalu, kati ya baraza na madhabahu, walikuwapo wanaume wapatao ishirini na watano. Wakiwa wamelipa kisogo Hekalu la BWANA na kuelekeza nyuso zao upande wa mashariki, wakilisujudia jua huko mashariki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo akanileta mpaka kwenye ukumbi wa ndani wa nyumba ya bwana, nako huko katika ingilio la Hekalu, kati ya baraza na madhabahu, walikuwepo wanaume wapatao ishirini na watano. Wakiwa wamelipa kisogo Hekalu la bwana na kuelekeza nyuso zao upande wa mashariki, wakilisujudia jua huko mashariki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akanileta mpaka ua wa ndani wa nyumba ya BWANA, na tazama, mlangoni pa hekalu la BWANA, kati ya ukumbi na madhabahu, walikuwako watu kama ishirini na watano, wamelipa kisogo hekalu la BWANA, na nyuso zao zimeelekea upande wa mashariki, nao wanaliabudu jua, kwa kuuelekea upande wa mashariki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akanipeleka mpaka ua wa ndani ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Huko mlangoni mwa hekalu, kati ya ukumbi na madhabahu, walikuwapo wanaume wapatao ishirini na watano, wakilipa kisogo hekalu, na nyuso zao zimeelekea upande wa mashariki. Walikuwa wanaabudu jua wakielekea upande wa mashariki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akanipeleka katika ua wa ndani wa Nyumba ya Bwana, nikaona hapo pa kuliingilia Jumba la Bwana katikati ya ukumbi na meza ya kutambikia waume kama 25, walikuwa wameligeuzia Jumba la Bwana migongo yao, lakini nyuso zilielekea upande wa maawioni kwa jua, wakiliangukia jua na kuyaelekea maawio yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akanileta mpaka ua wa ndani wa nyumba ya BWANA, na tazama, mlangoni pa hekalu la BWANA, kati ya ukumbi na madhabahu, walikuwako watu kama ishirini na watano, wamelipa kisogo hekalu la BWANA, na nyuso zao zimeelekea upande wa mashariki, nao wanaliabudu jua, kwa kuuelekea upande wa mashariki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akanipeleka mpaka katika uwanja wa ndani wa nyumba ya Yawe. Huko kwenye mulango wa hekalu, kati ya baraza na mazabahu, kulikuwa wanaume yapata makumi mbili na watano, wakigeuzia mugongo wao upande wa hekalu, na nyuso zao zikielekea upande wa mashariki. Walikuwa wanaabudu jua wakielekea upande wa mashariki.