Ezekiel 8:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilipotazama, nikaona maono: Kitu kilichofanana na binadamu. Sehemu yake ya chini, iliyoonekana kama ndio kiuno chake, ilikuwa kama moto. Toka kiuno chake kwenda juu alikuwa na mngao kama wa shaba ingaayo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikatazama, nikaona umbo mfano wa mwanadamu. Kutokana na kile kilichoonekana kuwa kiuno chake kuelekea chini alifanana na moto. Kuanzia kiuno kuelekea juu sura yake iling’aa vile chuma king’aavyo kikiwa ndani ya moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo nikaangalia, na tazama, kana kwamba ni mfano wa moto; tangu mfano wa viuno vyake na chini, moto; na tangu mfano wa viuno vyake na juu, kana kwamba ni mfano wa mwangaza, kama rangi ya kaharabu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilipotazama, nikaona maono: Kitu kilichofanana na binadamu. Sehemu yake ya chini, iliyoonekana kama ndio kiuno chake, ilikuwa kama moto. Toka kiuno chake kwenda juu alikuwa na mng'ao kama wa shaba ing'aayo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikatazama, nikaona umbo mfano wa mwanadamu. Kutokana na kile kilichoonekana kuwa kiuno chake kuelekea chini alifanana na moto. Kuanzia kwenye kiuno kuelekea juu sura yake kama chuma king'aavyo kikiwa ndani ya moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikatazama, nikaona umbo mfano wa mwanadamu. Kutokana na kile kilichoonekana kuwa kiuno chake kuelekea chini alifanana na moto. Kuanzia kwenye kiuno kuelekea juu sura yake kama chuma king’aavyo kikiwa ndani ya moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo nikaangalia, na tazama, palikuwa na kitu kilichofanana na mwanadamu; kuanzia kilichoonekana kama viuno vyake kwenda chini ilikuwa moto; na kuanzia kilichoonekana kama viuno vyake kwenda juu, ilikuwa mfano wa mwangaza, kama rangi ya kaharabu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilipotazama, nikaona maono: Kitu kilichofanana na binadamu. Sehemu yake ya chini, iliyoonekana kama ndio kiuno chake, ilikuwa kama moto. Toka kiuno chake kwenda juu alikuwa na mngao kama wa shaba ingaayo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipotazama nikaona, kama ni sura ya mtu; toka hapo palipokuwa kama kiuno mpaka chini ni moto, tena toka penye kiuno mpaka juu kulionekana kuwa kama kumetuka kulikokuwa kama kwa shaba iliyong'aa sana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo nikaangalia, na tazama, kana kwamba ni mfano wa moto; tangu mfano wa viuno vyake na chini, moto; na tangu mfano wa viuno vyake na juu, kana kwamba ni mfano wa mwangaza, kama rangi ya kaharabu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilipoangalia, nikaona kitu kilichofanana na mwanadamu. Sehemu yake ya chini, iliyoonekana kama ndio kiuno chake, ilikuwa kama moto. Toka kiuno chake kwenda juu alimetameta kama vile shaba.