Ezekiel 8:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, akanyosha kitu kama mkono, akanishika kwa nywele zangu. Roho ya Mungu ikaninyanyua kati ya ardhi na mbingu, ikanipeleka mpaka Yerusalemu nikiwa katika maono hayo ya Mungu. Nikafika kwenye kiingilio cha lango la ukumbi wa ndani linaloelekea upande wa kaskazini, mahali palipowekwa sanamu iliyomchukiza Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akanyoosha kitu kilichofanana na mkono, akaniinua kwa kushika nywele za kichwa changu. Roho wa Mungu akaniinua juu kati ya nchi na mbingu, na nikiwa katika maono ya Mungu, akanichukua hadi Yerusalemu, kwenye ingilio la lango la kaskazini mwa ukumbi wa ndani, mahali iliposimama ile sanamu inayochochea wivu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akanyosha mfano wa mkono, akanishika kwa kishungi kimoja cha nywele za kichwa changu; nayo roho ikaniinua kati ya dunia na mbingu, ikanileta katika maono ya Mungu mpaka Yerusalemu, mpaka mlango wa kuingilia ua wa ndani uelekeao upande wa kaskazini; mahali palipokuwa pamewekwa sanamu ya wivu, itiayo wivu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, akanyosha kitu kama mkono, akanishika kwa nywele zangu. Roho ya Mungu ikaninyanyua kati ya ardhi na mbingu, ikanipeleka mpaka Yerusalemu nikiwa katika maono hayo ya Mungu. Nikafika kwenye kiingilio cha lango la ukumbi wa ndani linaloelekea upande wa kaskazini, mahali palipowekwa sanamu iliyomchukiza Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akanyoosha kitu kilichoonekana kama mkono, akaniinua kwa kushika nywele za kichwa changu. Roho akaniinua juu kati ya nchi na mbingu nikiwa katika maono ya Mungu akanichukua mpaka Yerusalemu, kwenye ingilio la lango la upande wa kaskazini ya ukumbi wa ndani, mahali iliposimama ile sanamu ichocheayo wivu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akanyoosha kitu kilichoonekana kama mkono, akaniinua kwa kushika nywele za kichwa changu. Roho akaniinua juu kati ya nchi na mbingu nikiwa katika maono ya Mungu akanichukua mpaka Yerusalemu, kwenye ingilio la lango la upande wa kaskazini ya ukumbi wa ndani, mahali iliposimama ile sanamu ichocheayo wivu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akanyosha mfano wa mkono, akanishika kwa kishungi kimoja cha nywele za kichwa changu; nayo roho ikaniinua kati ya dunia na mbingu, ikanileta katika maono ya Mungu mpaka Yerusalemu, mpaka mlango wa kuingilia ua wa ndani uelekeao upande wa kaskazini; mahali palipokuwa pamewekwa sanamu ya wivu, itiayo wivu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, akanyosha kitu kama mkono, akanishika kwa nywele zangu. Roho ya Mungu ikaninyanyua kati ya ardhi na mbingu, ikanipeleka mpaka Yerusalemu nikiwa katika maono hayo ya Mungu. Nikafika kwenye kiingilio cha lango la ukumbi wa ndani linaloelekea upande wa kaskazini, mahali palipowekwa sanamu iliyomchukiza Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akakunjua kilichofanana na mkono, akanishika kishungi cha kichwani, upepo ukanichukua kuwa katikati ya nchi na ya mbingu, ukanipeleka Yerusalemu katika maono ya Kimungu pa kuliingilia lango la ndani lilioelekea kaskazini; ndipo, palipokuwa pamewekwa kinyago cha wivu kilichotia wivu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akanyosha mfano wa mkono, akanishika kwa kishungi kimoja cha nywele za kichwa changu; nayo roho ikaniinua kati ya dunia na mbingu, ikanileta katika maono ya Mungu mpaka Yerusalemu, mpaka mlango wa kuingilia ua wa ndani uelekeao upande wa kaskazini; mahali palipokuwa pamewekwa sanamu ya wivu, itiayo wivu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, akanyoosha kitu kinachokuwa kama vile mukono, akanikamatia kwa nywele zangu. Roho wa Mungu akaninyanyua kati ya dunia na mbingu, akanipeleka mpaka Yerusalema nikiwa katika maono hayo ya Mungu. Nikafika kwenye kiingilio cha mulango wa baraza ya ndani inayoelekea upande wa kaskazini, pahali palipowekwa sanamu iliyomuletea Mungu wivu.