Ezekiel 9:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu sita wakaja kutoka upande wa lango la juu linaloelekea kaskazini, kila mmoja na silaha yake ya kuangamiza mkononi mwake. Pamoja nao, alikuwapo mtu mmoja ambaye alikuwa amevaa mavazi ya kitani, naye ana kidau cha wino. Wakaingia ndani ya hekalu, wakasimama pembeni mwa madhabahu ya shaba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nami nikaona watu sita wakija toka upande wa lango la juu linalotazama kaskazini, kila mmoja akiwa na silaha za kuangamiza mkononi mwake. Kati yao palikuwa na mtu aliyevaa mavazi ya kitani safi, naye alikuwa na vifaa vya mwandishi kiunoni mwake. Wakaingia ndani ya Hekalu na kusimama pembeni mwa madhabahu ya shaba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, watu sita wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja ana kitu chake cha kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu sita wakaja kutoka upande wa lango la juu linaloelekea kaskazini, kila mmoja na silaha yake ya kuangamiza mkononi mwake. Pamoja nao, alikuwapo mtu mmoja ambaye alikuwa amevaa mavazi ya kitani, naye ana kidau cha wino. Wakaingia ndani ya hekalu, wakasimama pembeni mwa madhabahu ya shaba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nami nikaona watu sita wakija toka upande wa lango la juu, linalotazama kaskazini kila mmoja na silaha za kuangamiza mkononi mwake. Pamoja nao alikuwepo mtu aliyekuwa amevaa mavazi ya kitani safi, naye alikuwa na vifaa vya mwandishi akiwa amevishikilia upande mmoja. Wakaingia ndani ya Hekalu wakasimama pembeni mwa madhabahu ya shaba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nami nikaona watu sita wakija toka upande wa lango la juu, linalotazama kaskazini kila mmoja na silaha za kuangamiza mkononi mwake. Pamoja nao alikuwepo mtu aliyekuwa amevaa mavazi ya kitani safi, naye alikuwa na vifaa vya mwandishi akiwa amevishikilia upande mmoja. Wakaingia ndani ya Hekalu wakasimama pembeni mwa madhabahu ya shaba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, watu sita wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja akiwa na silaha yake ya kuua mkononi; na mtu mmoja kati yao akiwa amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu sita wakaja kutoka upande wa lango la juu linaloelekea kaskazini, kila mmoja na silaha yake ya kuangamiza mkononi mwake. Pamoja nao, alikuwapo mtu mmoja ambaye alikuwa amevaa mavazi ya kitani, naye ana kidau cha wino. Wakaingia ndani ya hekalu, wakasimama pembeni mwa madhabahu ya shaba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikaona watu sita, waliotokea katika njia ya lango la juu lililoelekea kaskazini, kila mtu alikuwa ameshika mkononi mwake chombo chake cha kupondea; lakini mtu mmoja aliyekuwa katikati yao alikuwa amevaa vazi la ukonge, napo kiunoni pake alikuwa na kichupa cha wino cha mwandishi, wakaja, wakasimama kando ya meza ya shaba ya kutambikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, watu sita wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja ana kitu chake cha kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu sita wakakuja kutoka upande wa mulango wa juu unaoelekea upande wa kaskazini, kila mumoja na silaha yake ya kuangamiza katika mukono wake. Pamoja nao, kulikuwa mutu mumoja ambaye alikuwa amevaa nguo ya kitani, naye ana chupa la wino. Wakaingia ndani ya hekalu, wakasimama pembeni ya mazabahu ya shaba.