Ezekiel 9:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha utukufu wa Mungu wa Israeli uliondoka pale juu ya kiumbe chenye mabawa na kupanda juu mpaka kizingiti cha nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa mavazi ya kitani, mwenye kidau cha wino,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi utukufu wa Mungu wa Israeli ukaondoka hapo juu ya makerubi, ulikokuwa umekaa, ukaenda kwenye kizingiti cha Hekalu. Ndipo Mwenyezi Mungu akamwita yule mtu aliyevaa kitani safi na mwenye vifaa vya mwandishi kiunoni mwake,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na huo utukufu wa Bwana wa Israeli ulikuwa umepanda juu kutoka kwa kerubi, ambaye ulikuwa juu yake, mpaka kizingiti cha nyumba; akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa bafta, mwenye kidau cha wino cha mwandishi kiunoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha utukufu wa Mungu wa Israeli uliondoka pale juu ya kiumbe chenye mabawa na kupanda juu mpaka kizingiti cha nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa mavazi ya kitani, mwenye kidau cha wino,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi utukufu wa Mungu wa Israeli ukaondoka hapo juu ya makerubi, ulikokuwa umekaa, ukaenda kwenye kizingiti cha Hekalu. Ndipo BWANA akamwita yule mtu aliyevaa kitani safi aliyekuwa na vifaa vya mwandishi akiwa amevishikilia upande wake mmoja,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi utukufu wa Mungu wa Israeli ukaondoka hapo juu ya makerubi, ulikokuwa umekaa, ukaenda kwenye kizingiti cha Hekalu. Ndipo bwana akamwita yule mtu aliyevaa kitani safi aliyekuwa na vifaa vya mwandishi akiwa amevishikilia upande wake mmoja,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na huo utukufu wa Bwana wa Israeli ulikuwa umepanda juu kutoka kwa kerubi, ambaye ulikuwa juu yake, mpaka kizingiti cha nyumba; akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa bafta, mwenye kidau cha wino cha mwandishi kiunoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha utukufu wa Mungu wa Israeli uliondoka pale juu ya kiumbe chenye mabawa na kupanda juu mpaka kizingiti cha nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa mavazi ya kitani, mwenye kidau cha wino,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, utukufu wa Mungu wa Isiraeli ulipoondoka kwenye Kerubi, ulikokuwa, ukaja kwenye kizingiti cha mlango wa hiyo nyumba, akamgutia yule mtu aliyevaa vazi la ukonge, aliyekuwa na kichupa cha wino cha mwandishi kiunoni pake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na huo utukufu wa Bwana wa Israeli ulikuwa umepanda juu kutoka kwa kerubi, ambaye ulikuwa juu yake, mpaka kizingiti cha nyumba; akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa bafta, mwenye kidau cha wino cha mwandishi kiunoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha utukufu wa Mungu wa Israeli uliondoka pale juu ya makerubi na kupanda juu mpaka kwenye kizingiti cha nyumba ya Yawe. Yawe akamwita mutu yule aliyekuwa amevaa nguo ya kitani, mwenye chupa la wino,