Ezekiel 9:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akamwambia, “Pita katikati ya mji wa Yerusalemu, ukatie alama kwenye vipaji vya nyuso za watu wanaohuzunika na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayotendeka katika mji huu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
akamwambia, “Pita katika mji wote wa Yerusalemu ukaweke alama kwenye paji za nyuso za wale watu wanaohuzunika na kuomboleza kwa sababu ya machukizo yote yanayotendeka katika mji huu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akamwambia, “Pita katikati ya mji wa Yerusalemu, ukatie alama kwenye vipaji vya nyuso za watu wanaohuzunika na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayotendeka katika mji huu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
akamwambia, “Pita katika mji wote wa Yerusalemu ukaweke alama juu ya vipaji vya nyuso za wale watu wanaohuzunika na kuomboleza kwa sababu ya machukizo yote yanayotendeka katika mji huu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
akamwambia, “Pita katika mji wote wa Yerusalemu ukaweke alama juu ya vipaji vya nyuso za wale watu wanaohuzunika na kuomboleza kwa sababu ya machukizo yote yanayotendeka katika mji huu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso za watu wanaopiga kite na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akamwambia, “Pita katikati ya mji wa Yerusalemu, ukatie alama kwenye vipaji vya nyuso za watu wanaohuzunika na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayotendeka katika mji huu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akamwambia: Pitia humu mjini katikati, humu Yerusalemu katikati, uwaandike kichoro mapajini wale watu wapigao kite na kuyaugulia hayo machukizo yote yafanyikayo humu mjini!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
akamwambia hivi: Pita katikati ya Yerusalema, upate kutia kitambulisho kwenye vipaji vya nyuso za watu wanaohuzunika na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayotendeka katika muji huu.