Ezekiel 9:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waueni wazee papo hapo, wavulana kwa wasichana, watoto na wanawake; lakini kila mmoja mwenye alama, msimguse. Anzeni katika maskani yangu.” Basi, wakaanza na wazee waliokuwa mbele ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waueni wazee, vijana wa kiume na wa kike, wamama na watoto, lakini msimguse mtu yeyote mwenye alama. Anzieni katika mahali pangu patakatifu.” Kwa hiyo wakaanza na wale wazee waliokuwa mbele ya Hekalu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waueni wazee papo hapo, wavulana kwa wasichana, watoto na wanawake; lakini kila mmoja mwenye alama, msimguse. Anzeni katika maskani yangu.” Basi, wakaanza na wazee waliokuwa mbele ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waueni wazee, vijana wa kiume na wa kike, wanawake na watoto, lakini msimguse mtu ye yote mwenye alama. Anzieni katika mahali pangu patakatifu.” Kwa hiyo wakaanza na wale wazee waliokuwa mbele ya Hekalu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waueni wazee, vijana wa kiume na wa kike, wanawake na watoto, lakini msimguse mtu yeyote mwenye alama. Anzieni katika mahali pangu patakatifu.” Kwa hiyo wakaanza na wale wazee waliokuwa mbele ya Hekalu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Waueni kabisa, wazee, na viijana, na wasichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu yeyote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waueni wazee papo hapo, wavulana kwa wasichana, watoto na wanawake; lakini kila mmoja mwenye alama, msimguse. Anzeni katika maskani yangu.” Basi, wakaanza na wazee waliokuwa mbele ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wazee, wasichana, wavulana, watoto, wanawake, waueni wote pia, waangamie! Lakini kila mtu mwenye kichoro msimguse kabisa! Anzieni hapa Patakatiu pangu! Wakawanzia wale wazee waliokuwa mbele ya hiyo Nyumba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muwaue wazee palepale, vijana wanaume na wabinti, watoto na wanawake; lakini kila mumoja mwenye kuwa na kitambulisho, musimuguse. Muanzie katika hekalu langu. Basi, wakaanza na wazee waliokuwa mbele ya nyumba ya Yawe.