Ezekiel 9:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati walipokuwa wakiwaua, mimi niliachwa peke yangu, nikaanguka kifudifudi, nikalia, “Ee Bwana Mwenyezi-Mungu, je, utaangamiza watu wote wa Israeli waliobaki, ukitimiza ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipokuwa wakiwaua watu, nami nikaachwa peke yangu, nilisujudu, nikapaza sauti na kusema, “Ee Bwana Mungu Mwenyezi! Je, utaangamiza mabaki yote ya Israeli, katika kumwagwa huku kwa ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena ikawa, walipokuwa wakipiga, nami nikiachwa, nalianguka kifudifudi, nikalia, nikasema, Ee Bwana MUNGU! Utaangamiza mabaki yote ya Israeli, wakati wa kumwaga ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati walipokuwa wakiwaua, mimi niliachwa peke yangu, nikaanguka kifudifudi, nikalia, “Ee Bwana Mwenyezi-Mungu, je, utaangamiza watu wote wa Israeli waliobaki, ukitimiza ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati walipokuwa wanaua watu, mimi nilikuwa nimeachwa peke yangu, nikaanguka kifudifudi, nikapiga kelele nikisema, “Ee BWANA Mwenyezi! Je, utaangamiza mabaki yote ya Israeli, katika kumwagwa huku kwa ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati walikuwa wakiwaua watu, nami nilikuwa nimeachwa peke yangu, nikaanguka kifudifudi, nikapiga kelele nikisema, “Ee bwana Mwenyezi! Je, utaangamiza mabaki yote ya Israeli, katika kumwagwa huku kwa ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena ikawa, walipokuwa wakiwaua, nami nikaachwa, nilianguka kifudifudi, nikalia, nikasema, Ee Bwana MUNGU! Utaangamiza mabaki yote ya Israeli, wakati wa kumwaga ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati walipokuwa wakiwaua, mimi niliachwa peke yangu, nikaanguka kifudifudi, nikalia, “Ee Bwana Mwenyezi-Mungu, je, utaangamiza watu wote wa Israeli waliobaki, ukitimiza ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa walipokwenda kuwapiga watu vivyo, hivyo, mimi nikasalia hapo peke yangu; ndipo, nilipoanguka kifudifudi, nikalia nikisema: E Bwana Mungu, wewe utayaangamiza masao yote ya Isiraeli, ukiumwagia Yerusalemu makali yako yenye moto?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena ikawa, walipokuwa wakipiga, nami nikiachwa, nalianguka kifudifudi, nikalia, nikasema, Ee Bwana MUNGU! Utaangamiza mabaki yote ya Israeli, wakati wa kumwaga ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati walipokuwa wakiwaua, mimi niliachwa peke yangu, nikaanguka uso mpaka chini, nikalia: Ee Bwana wangu Yawe, utaangamiza watu wote wa Israeli waliobaki, ukitimiza kasirani yako juu ya Yerusalema?