Ezra 1:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vyombo vyote vya dhahabu na fedha, pamoja na vitu vinginevyo vilikuwa jumla yake 5,400. Vyote hivi, Sheshbaza alivichukua hadi Yerusalemu wakati yeye pamoja na watu wengine alipotolewa uhamishoni Babuloni kwenda Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa jumla, kulikuwa na vyombo elfu tano na mia nne vya dhahabu na vya fedha. Sheshbaza akavileta hivi vyote wakati watu walipotoka uhamishoni Babeli kwenda Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Vyombo vyote vya dhahabu na vya fedha vilikuwa jumla yake elfu tano na mia nne. Hivyo vyote Sheshbaza akakwea navyo, hapo walipokwea wale wa uhamisho kutoka Babeli mpaka Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vyombo vyote vya dhahabu na fedha, pamoja na vitu vinginevyo vilikuwa jumla yake 5,400. Vyote hivi, Sheshbaza alivichukua hadi Yerusalemu wakati yeye pamoja na watu wengine alipotolewa uhamishoni Babuloni kwenda Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa ujumla, kulikuweko na vyombo 5,400 vya dhahabu na vya fedha. Sheshbaza akavileta hivi vyote wakati watu walipotoka uhamishoni Babeli kwenda Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa ujumla, kulikuwa na vyombo 5,400 vya dhahabu na vya fedha. Sheshbaza akavileta hivi vyote wakati watu walipotoka uhamishoni Babeli kwenda Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Vyombo vyote vya dhahabu na vya fedha vilikuwa jumla yake elfu tano na mia nne. Hivyo vyote Sheshbaza akakwea navyo, hapo walipokwea wale wa uhamisho kutoka Babeli mpaka Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vyombo vyote vya dhahabu na fedha, pamoja na vitu vinginevyo vilikuwa jumla yake 5,400. Vyote hivi, Sheshbaza alivichukua hadi Yerusalemu wakati yeye pamoja na watu wengine alipotolewa uhamishoni Babuloni kwenda Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vyombo vyote vya dhahabu na vya fedha vilikuwa 5400. Hivi vyote Sesebasari alikwenda navyo, wale waliotekwa na kuhamishwa walipotoka Babeli kwenda kupanda Yerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Vyombo vyote vya dhahabu na vya fedha vilikuwa jumla yake elfu tano na mia nne. Hivyo vyote Sheshbaza akakwea navyo, hapo walipokwea wale wa uhamisho kutoka Babeli mpaka Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vyombo vyote vya zahabu na feza, pamoja na vitu vingine vilikuwa jumla yake elfu tano mia ine. Vyote hivi, Sesebasari alivibeba mpaka Yerusalema wakati yeye pamoja na watu wengine walipotolewa toka katika uhamisho kule Babeli kwenda Yerusalema.