Ezra 1:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakaondoka viongozi wa koo za makabila ya Yuda na Benyamini, makuhani na Walawi, na kila mtu ambaye Mungu alimpa moyo wa kwenda kujenga upya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, iliyoko Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha viongozi wa jamaa ya Yuda na Benyamini na makuhani na Walawi kila mmoja ambaye moyo wake ulisukumwa na Mungu, akajiandaa kupanda ili kuijenga nyumba ya Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo wakaondoka wakuu wa mbari za mababa, wa Yuda na Benyamini, na makuhani, na Walawi, naam, watu wote ambao Mungu amewaamsha roho zao kukwea, ili kuijenga nyumba ya Bwana, iliyoko Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakaondoka viongozi wa koo za makabila ya Yuda na Benyamini, makuhani na Walawi, na kila mtu ambaye Mungu alimpa moyo wa kwenda kujenga upya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, iliyoko Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha viongozi wa jamaa ya Yuda na Benyamini na makuhani na Walawi kila mmoja ambaye moyo wake ulisukumwa na Mungu, akajiandaa kupanda ili kuijenga nyumba ya BWANA huko Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha viongozi wa jamaa ya Yuda na Benyamini na makuhani na Walawi kila mmoja ambaye moyo wake ulisukumwa na Mungu, akajiandaa kupanda ili kuijenga nyumba ya bwana huko Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo wakaondoka wakuu wa koo za mababa, wa Yuda na Benyamini, na makuhani, na Walawi, naam, watu wote ambao Mungu ameamsha roho zao kukwea, ili kuijenga nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakaondoka viongozi wa koo za makabila ya Yuda na Benyamini, makuhani na Walawi, na kila mtu ambaye Mungu alimpa moyo wa kwenda kujenga upya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, iliyoko Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wao waliokuwa vichwa vya milango ya Yuda na ya Benyamini pamoja na watambikaji na Walawi walioamshwa roho zao na Mungu wakaondoka kwenda kuijenga Nyumba ya Bwana iliyoko Yerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo wakaondoka wakuu wa mbari za mababa, wa Yuda na Benyamini, na makuhani, na Walawi, naam, watu wote ambao Mungu amewaamsha roho zao kukwea, ili kuijenga nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, viongozi wa ukoo za makabila ya Yuda na Benjamina wakaondoka, makuhani na Walawi, na kila mutu ambaye Mungu alimupa moyo wa kwenda kujenga upya nyumba ya Yawe, inayokuwa Yerusalema.