Ezra 1:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Koreshi aliwarudishia vyombo ambavyo mfalme Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu na kuviweka katika nyumba ya miungu yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya hayo, Mfalme Koreshi akavitoa vyombo vilivyokuwa mali ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, ambavyo Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka Yerusalemu na kuviweka katika hekalu la mungu wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena Koreshi, mfalme, alivitoa vyombo vya nyumba ya Bwana, alivyokuwa amevileta Nebukadreza
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Koreshi aliwarudishia vyombo ambavyo mfalme Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu na kuviweka katika nyumba ya miungu yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaidi ya hayo, Mfalme Koreshi akavitoa vyombo vilivyokuwa mali ya Hekalu la BWANA, ambavyo Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka Yerusalemu na kuviweka katika hekalua la mungu wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya hayo, Mfalme Koreshi akavitoa vyombo vilivyokuwa mali ya Hekalu la bwana, ambavyo Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka Yerusalemu na kuviweka katika hekalu la mungu wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena Koreshi, mfalme, alivitoa vyombo vya nyumba ya BWANA, alivyokuwa amevileta Nebukadneza toka Yerusalemu, na kuvitia katika nyumba ya miungu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Koreshi aliwarudishia vyombo ambavyo mfalme Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu na kuviweka katika nyumba ya miungu yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mfalme Kiro akavitoa vyombo vyote vya Nyumba ya Bwana, Nebukadinesari alivyovitoa Yerusalemu na kuvitia jumbani mwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena Koreshi, mfalme, alivitoa vyombo vya nyumba ya BWANA, alivyokuwa amevileta Nebukadreza toka Yerusalemu, na kuvitia katika nyumba ya miungu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Kiro akawarudishia vyombo ambavyo mufalme Nebukadneza alikuwa amevitwaa kutoka katika nyumba ya Yawe na kuviweka katika nyumba ya miungu yake.