Ezra 10:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati Ezra alipokuwa anaomba na kuungama huku analia na kujiangusha kifudifudi mbele ya nyumba ya Mungu, umati mkubwa wa watu wa Israeli, wanaume, wanawake na watoto, walikusanyika karibu naye wakilia kwa uchungu mwingi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ezra alipokuwa anaomba na kuungama, huku akilia na kujitupa chini mbele ya nyumba ya Mungu, umati mkubwa wa Waisraeli wakiwemo wanaume, wanawake na watoto walikusanyika kumzunguka. Nao pia wakalia sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi hapo Ezra alipokuwa akiomba na kuungama, akilia, na kujiangusha kifudifudi mbele ya nyumba ya Mungu, wakamkusanyikia katika Israeli wote kusanyiko kubwa sana la wanaume, na wanawake, na watoto; maana watu hao walikuwa wakilia sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati Ezra alipokuwa anaomba na kuungama huku analia na kujiangusha kifudifudi mbele ya nyumba ya Mungu, umati mkubwa wa watu wa Israeli, wanaume, wanawake na watoto, walikusanyika karibu naye wakilia kwa uchungu mwingi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Ezra alipokuwa anaomba na kuungama, huku akilia na kujitupa chini mbele ya nyumba ya Mungu, umati mkubwa wa Waisraeli, wanaume, wanawake na watoto walikusanyika kumzunguka. Nao pia wakalia sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati Ezra alipokuwa anaomba na kuungama, huku akilia na kujitupa chini mbele ya nyumba ya Mungu, umati mkubwa wa Waisraeli, wanaume, wanawake na watoto walikusanyika kumzunguka. Nao pia wakalia sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi hapo Ezra alipokuwa akiomba na kuungama, akilia, na kujiangusha kifudifudi mbele ya nyumba ya Mungu, kusanyiko kubwa sana la wanaume, wanawake na watoto, kutoka katika Israeli likamkusanyikia; maana watu hao walikuwa wakilia sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati Ezra alipokuwa anaomba na kuungama huku analia na kujiangusha kifudifudi mbele ya nyumba ya Mungu, umati mkubwa wa watu wa Israeli, wanaume, wanawake na watoto, walikusanyika karibu naye wakilia kwa uchungu mwingi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ezera alipoomba na kuungama hivyo akilia na kujiangusha chini mbele ya Nyumba ya Mungu, ndipo, walipokusanyika kwake Waisiraeli, ukawa mkutano mkubwa mno, waume na wake na wana, nao hao watu wakalia kilio kikubwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi hapo Ezra alipokuwa akiomba na kuungama, akilia, na kujiangusha kifudifudi mbele ya nyumba ya Mungu, wakamkusanyikia katika Israeli wote kusanyiko kubwa sana la wanaume, na wanawake, na watoto; maana watu hao walikuwa wakilia sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati Ezra alipokuwa anaomba na kuungama naye akilia na kujiangusha uso mpaka chini mbele ya nyumba ya Mungu, kundi kubwa la watu wa Israeli, wanaume, wanawake na watoto, wakakusanyika karibu naye wakilia kwa uchungu mwingi.