Ezra 10:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Afadhali maofisa wetu wabaki Yerusalemu kushughulikia jambo hili kwa niaba ya watu wote. Kisha, kila mmoja ambaye ameoa mwanamke wa kigeni na aje kwa zamu pamoja na viongozi na mahakimu wa mji wake, mpaka hapo ghadhabu kali ya Mungu wetu itakapoondolewa kwetu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maafisa wetu na watende kwa niaba ya kusanyiko lote. Kisha kila mmoja katika miji yetu ambaye ameoa mwanamke wa kigeni aje kwa wakati uliopangwa, akiwa pamoja na wazee na waamuzi wa kila mji, hadi hasira kali ya Mungu wetu katika shauri hili itakapoondolewa kwetu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi maakida wetu na wawekwe kwa ajili ya mkutano wote, na watu wote walio katika miji yetu, waliooa wanawake wageni, na waje nyakati zilizoamriwa, tena pamoja nao na waje wazee wa kila mji, na makadhi wa miji hiyo, hata ghadhabu kali ya Mungu wetu itakapotuondokea mbali, jambo hili likamalizike.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Afadhali maofisa wetu wabaki Yerusalemu kushughulikia jambo hili kwa niaba ya watu wote. Kisha, kila mmoja ambaye ameoa mwanamke wa kigeni na aje kwa zamu pamoja na viongozi na mahakimu wa mji wake, mpaka hapo ghadhabu kali ya Mungu wetu itakapoondolewa kwetu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maafisa wetu na wafanye kwa niaba ya kusanyiko lote. Kisha kila mmoja katika miji yetu ambaye ameoa mwanamke wa kigeni aje kwa wakati uliopangwa, akiwa pamoja na wazee na waamuzi wa kila mji, hadi hasira kali ya Mungu wetu katika shauri hili itakapoondolewa kwetu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maafisa wetu na wafanye kwa niaba ya kusanyiko lote. Kisha kila mmoja katika miji yetu ambaye ameoa mwanamke wa kigeni aje kwa wakati uliopangwa, akiwa pamoja na wazee na waamuzi wa kila mji, hadi hasira kali ya Mungu wetu katika shauri hili itakapoondolewa kwetu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakuu wetu na wawekwe kwa ajili ya mkutano wote, na watu wote walio katika miji yetu, waliooa wanawake wageni, na waje nyakati zilizoamriwa, tena pamoja nao na waje wazee wa kila mji, na waamuzi wa miji hiyo, hata ghadhabu kali ya Mungu wetu itakapoondolewa mbali, jambo hili likamalizike.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Afadhali maofisa wetu wabaki Yerusalemu kushughulikia jambo hili kwa niaba ya watu wote. Kisha, kila mmoja ambaye ameoa mwanamke wa kigeni na aje kwa zamu pamoja na viongozi na mahakimu wa mji wake, mpaka hapo ghadhabu kali ya Mungu wetu itakapoondolewa kwetu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakuu wetu na waondokee kuupigia mkutano wote shauri hili, kisha wote waliooa wanawake wageni mijini mwetu na waje siku zitakazowekwa; tena pamoja nao na waje hata wazee na waamuzi wa kila mji, mpaka watakapoyatuliza makali hayo ya Mungu wetu yawakayo moto kwa ajili ya jambo hili, yakatuacha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi maakida wetu na wawekwe kwa ajili ya mkutano wote, na watu wote walio katika miji yetu, waliooa wanawake wageni, na waje nyakati zilizoamriwa, tena pamoja nao na waje wazee wa kila mji, na makadhi wa miji hiyo, hata ghadhabu kali ya Mungu wetu itakapotuondokea mbali, jambo hili likamalizike.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Afazali wakubwa wetu wabaki Yerusalema kushugulikia jambo hili kwa ajili ya watu wote. Kisha, kila mumoja ambaye ameoa mwanamuke wa kigeni akuje kwa zamu pamoja na viongozi na waamuzi wa muji wake, mpaka pale kasirani kali ya Mungu wetu itakapoondolewa kwetu.”