Ezra 2:65 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mbali na hao, kulikuwa na watumishi wanaume na wanawake 7337; na walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake, wote 200.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
tena zaidi ya hao walikuwa na watumwa wa kiume na wa kike elfu saba, mia tatu na thelathini na saba (7,337); pia walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake mia mbili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
tena, zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao waume kwa wake, ambao walikuwa saba elfu, na mia tatu na thelathini na saba; nao walikuwa na waimbaji waume kwa wake mia mbili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mbali na hao, kulikuwa na watumishi wanaume na wanawake 7,337; na walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake, wote 200.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
pamoja na hao kulikuwapo na watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwapo waimbaji wanaume na wanawake 200.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
tena, zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao wa kiume na wa kike, ambao walikuwa elfu saba, na mia tatu na thelathini na saba; nao walikuwa na waimbaji wa kiume na wa kike mia mbili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mbali na hao, kulikuwa na watumishi wanaume na wanawake 7337; na walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake, wote 200.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
pasipo watumwa na vijakazi wao, nao walikuwa 7337; tena walikuwako waimbaji wa kiume na wa kike 200.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
tena, zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao waume kwa wake, ambao walikuwa saba elfu, na mia tatu na thelathini na saba; nao walikuwa na waimbaji waume kwa wake mia mbili.