Ezra 2:69 — Compare Translations

10 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walitoa kila mtu kadiri ya uwezo wake kwa ajili ya kazi hii. Jumla ya matoleo hayo ilikuwa kilo 500 za dhahabu, kilo 2,800 za fedha na mavazi 100 kwa ajili ya makuhani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni elfu sitini na moja za dhahabu, mane elfu tano za fedha, na mavazi mia moja ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakatoa kadiri walivyoweza, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walitoa kila mtu kadiri ya uwezo wake kwa ajili ya kazi hii. Jumla ya matoleo hayo ilikuwa kilo 500 za dhahabu, kilo 2,800 za fedha na mavazi 100 kwa ajili ya makuhani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,000 za dhahabu, mane 5,000 za fedha na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hii.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,000 za dhahabu, mane 5,000 za fedha, na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakatoa kadiri walivyoweza, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu elfu sitini na moja, na mane za fedha elfu tano, na mavazi mia moja ya makuhani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walitoa kila mtu kadiri ya uwezo wake kwa ajili ya kazi hii. Jumla ya matoleo hayo ilikuwa kilo 500 za dhahabu, kilo 2,800 za fedha na mavazi 100 kwa ajili ya makuhani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo, walivyoweza, wakatoa vipaji vyao, wakavitia katika kilimbiko cha jengo: vipande vya dhahabu vilivyoitwa Dariko 61000, ndio shilingi kama milioni mbili na 440000 na vipande vya fedha vilivyoitwa Mane 5000, ndio shilingi kama milioni, na mavazi ya watambikaji 100.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakatoa kadiri walivyoweza, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu sitini na moja elfu, na mane za fedha elfu tano, na mavazi mia ya makuhani.